Snoop Dogg Afurahishwa na Wimbo wa ‘Naanzaje’ ya Diamond Platnumz

[Picha: Naanzaje YouTube Video]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika nchini Tanzania Diamond Platnumz ameendelea kuchana mawimbi kwenye anga la muziki wa kimataifa baada ya rapa Snoop Dog kuweka picha ya video ya ‘Naanzaje’ kwenye akaunti yake Instagram.

Snoop Dogg ambaye ni moja kati ya marapa wanaoheshimika sana nchini Marekani alitumia ukurasa wake wa Instagram kwenye uwanja wa Instastory ambapo alichapisha picha ya Diamond Platnumz inayomuonesha akiwa kwenye video ya ‘Naanzaje’.

Soma Pia: Diamond Aeleza Sababu ya kuachia Wimbo Wake Mpya 'Naanzaje'

 Wengi wameshuku kuwa ‘Naanzaje’ huenda ndio wimbo pendwa wa Snoop Dogg kutoka kwa Diamond Platnumz kwani hiyo ni mara ya kwanza ya msanii huyo kuchapisha chochote kinachohusu kazi ya Diamond Platnumz kwenye akaunti yake tangu wakutane takribani wiki saba nyuma.

Sio Snoop Dogg pekee ambaye ameonekana kupenda ngoma hiyo ya Diamond Platnumz bali hata mashabiki wa muziki ndani na nje ya Tanzania wamepokea video ya ngoma hiyo kwa ukubwa.

Soma Pia: Zuchu Ajivunia Kutokana na Mafanikio Yake Makubwa Kimuziki

Kwenye mtandao wa YouTube, video ya ‘Naanzaje’ imeweka rekodi mpya baada ya kutazamwa mara Laki Moja ndani ya dakika 40 tu tangu kuachiwa kwake, rekodi ambayo mwanzoni ilishikiliwa na Harmonize kupitia video yake ya ‘Attitude’ iliyotazamwa mara Laki moja ndani ya dakika 44 tu.

Aidha video ya ‘Naanzaje’ ilitazamwa mara milioni moja ndani ya masaa 13 na hii imefanya ‘Waah’ iliyotazamwa mara Milioni moja ndani ya saa manane kuwa video iliyofikisha views milioni moja ndani ya muda mfupi kuliko video zote nchini Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=iKbW2EDs_mE

Leave your comment