Harmonize Amkaribisha Ibraah Kwenye Tour Yake ya Marekani

[Picha: SoundCity TV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Lebo ya Konde Gang huwa haina jambo dogo na hiyo imethibitishwa hivi karibuni baada ya bosi wa Konde Gang Harmonize kumjumuisha Ibraah kwenye tour yake ambayo inatarajiwa kurindima huko nchini Marekani itakayoanza Septemba 4.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Video ya ‘Teacher’

Harmonize aliweka wazi taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram baada ya kuandika "My people in USA we got my brother Chinga Ibraah special one the king of new school coming with me on my tour"

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Ibraah kwenda kufanya onesho la muziki nchini Marekani na taarifa hizo kutoka kwa Harmonize zilionekana kumfurahisha sana Ibraah ambaye nae alichapisha ujumbe mrefu kwa Harmonize kwa kuandika.

"Thank God may you bless this trip I believe that you exist zidi kunipa nguvu na furaha ili nizidi kufanya vitu vingi zaidi."

Soma Pia: Harmonize Atangaza Ujio wa Konde Gang Radio na TV

Harmonize anatarajiwa kufanya tour hiyo kwa takriban miezi mitatu na atafanya maonesho kwenye majiji kama Ohio, Houston, Phoenix, Las Vegas, New York, Los Angeles, Salt Lake City, Atlanta na Syracruse kwa nchini Marekani na kwa Ulaya atatumbuiza nchini Denmark na Sweden na kisha Januari atamaliza tour hiyo huko Sierra Leone.

Kando na Harmonize, Diamond Platnumz hivi karibuni pia ametangaza kuwa na ziara yake nchini Marekani ambayo itaanza Oktoba 8 mwaka huu kwenye jiji la Atlanta na kisha kuendelea kwenye miji mengine.

Leave your comment