Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Video ya ‘Teacher’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi wa lebo ya Konde Gang Harmonize ameachia video ya ngoma yake mpya ‘Teacher’.

Tofauti na video nyingi zinatoka hivi sasa, video ya ‘Teacher’ imefanyika kwenye mazingira ya kijijini na Harmonize anaonekana akiwa amevaa barakoa kwenye baadhi ya vipande vya video kama alivyofanya kwenye video yake ya ‘Sandakalawe’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa Tanzania na Harmonize, Rich Mavoko, Mabantu na Mr Blue

Director wa video hii bila shaka ameonesha uafrika halisi kwenye video hii kwa kutumia watu waliovaa mavazi ya kiasili na ya kimaasai.

Pumzi ya video yoyote ya Amapiano iko kwenye dansi na Harmonize hajafanya ajizi kwenye eneo hili kwani ameweza kutumia vyema wacheza dansi wake ambao baadhi wamevaa mavazi ya kiafrika kabisa kama vitenge na batiki, huku wadada warembo wanaonekana wakiwa wamevaa sare ambazo zimevutia sana.

Kwenye mtandao wa YouTube, dakika chache baada ya Harmonize kuachia video hii namba ya watazamaji (views) zilionekana kuganda kwa muda mrefu jambo ambalo lilizua taharuki kwa mashabiki na Harmonize alitumia akaunti yake ya Instagram kuonesha kushangazwa kwake.

Soma Pia: Harmonize Amuomba Ibraah Ampe Nafasi Avume YouTube

Harmonize aliandika: "God is good imefika wakati Konde Boy akiachia ngoma hata YouTube wenyewe inashangaa hiki ni nini hadi inastak kuhesabu. Lets see kinatokea nini maana sijawahi ona …."

Kwa sasa speed ya views imerejea kwenye hali yake ya kawaida, na kufikia sasa video hiyo imeshatazamwa mara laki mbili hamsini na tatu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=mPVoKSc6LJo

Leave your comment