Harmonize Amuomba Ibraah Ampe Nafasi Avume YouTube

[Picha: Juniortz.com]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wimbo wa 'Jipinde' kutoka kwa msanii Ibraah umekuwa ukivuma sana mtandaoni. Kando na ngoma hiyo kumuandikishia Ibraah rekodi ya kupata watazamaji wengi sana ndani ya muda mfupi, 'Jipinde' vilevile ilipiku ngoma mingi mtandaoni na kuchukua nafasi ya kwanza kwenye orodha ya nyimbo bora kwenye YouTube Tanzania.

Soma Pia: Nyimbo 5 Mpya za Rayvanny, Alikiba, Ibraah, Zuchu na Harmonize Zinazotamba Tanzania Wiki Hii

Mkurugenzi mkuu wa Konde Music Worldwide Harmonize, ambaye pia ni bosi wake Ibraah, alitoa ngoma yake iitwayo 'Teacher' siku chache baada ya Ibraah kutoa 'Jipinde'. Ngoma yake Harmonize, hata hivyo, haikuipiku 'Jipinde', jambo ambolo limemfanya Harmonize kupitia mitandao ya kijamii kumuomba Ibraah nafasi ya kuipisha ngoma yake ya 'Teacher' kusudi yeye pia aweze kuvuma.

Harmonize katika ujumbe wake alisema kuwa Ibraah alikuwa amemshinda kila mtu, ila yeye alikuwa na ombi tu la kupishwa.

"Brother naomba uniache niingie number one trend maana kila mtu kakushindwa sio vijana sio watu wazima au mpaka tukuitie (Hamza),”Harmonize aliandika mtandaoni.

Ibraah katika jibu lake alisema kuwa ili msanii avume katika mtandao wa YouTube, basi atalazimika aimbe na wala sio kupiga kelele.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia ‘Teacher’

"@harmonize_tz kalibu sana kijana kutoka koo ya kiume #chamalawana. Katika mji wangu wa YouTube masharti ni madogo sana usipige kelele imba," Ibraah alijibu.

Ibraah ni mojawapo wa wasanii kutoka lebo ya Konde Music Worldwide ambao wanafanya vizuri sana na kazi zao zimepokelewa vyema na mashabiki. Ibraah amepata wafuasi wengi sana mtandaoni na umaarafu mkubwa.

Leave your comment