Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia ‘Teacher’

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Harmonize ameachia wimbo mpya wenye jina ‘Teacher’.

Kama ilivyokuwa kwa nyimbo zake mbili za mwisho ‘Sandakalawe’ pamoja na ‘Mang'dakiwe Remix’, wimbo huu pia umefuata mahadhi ya Amapiano na hii inamfanya Harmonize kuwa na nyimbo nyingi zaidi za Amapiano nyuma ya Damian Soul.

Soma Pia: Harmonize Afichua Sababu Iliyomfanya Kuanzisha Lebo ya Konde Music Worldwide

Kwenye wimbo huu, Harmonize anaongelea mambo tofauti yanayohusu muziki kama vile washindani wake wa kwenye muziki, ugumu wa kwenye maisha, kiki za kwenye muziki na pia ametumia kibao hiki kudokeza namna ambavyo muziki unamkubali.

Kwenye aya ya kwanza ya wimbo huu Harmonize anaimba "Ninachojua masela huko mtaani kuna dhiki ndo maana singishi hela wala nnavyovimiliki mafumbo andika kwa dela watu wanataka muziki."

Mstari huu wa kwenye wimbo unaakisi hali ilivyo kwa sasa kwenye muziki wa Bongo Fleva kwani wasanii wengi wameonekana kupenda kuonesha utajiri wao.

Soma Pia: Harmonize Amtaja Ibraah Kama Mfalme wa Muziki wa Kizazi Kipya

Kwenye kiitikio Harmonize anatamba kisawasawa namna ambavyo ana uwezo wa kutawala kwenye muziki kwa kuimba "Huu muziki na uweza nauweza kuuimba na kucheza ona unavyonipendeza hadi majirani wameanza kunigeza."

Kwa mashabiki wanaomfuatilia Harmonize, bila shaka watakumbuka kuwa msanii huyo alidokeza ya ujio wa wimbo huo kupitia akaunti yake ya Instagram Agosti 12, baada ya kuchapisha video akiwa na timu yake studio wakicheza na kufurahia wimbo huo.

Wimbo huu umeandaliwa na mtayarishaji wa muziki Steve Spesho.

https://www.youtube.com/watch?v=seUsUJ3JCXs

Leave your comment