Tunda Man Ajibu Madai ya Uhasama Baina Yake na Diamond Platnumz

[Picha: Tunda Man and Diamond Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki maarufu nchini Tanzania Tunda Man amejitokeza na kujibu tuhuma kuwa kuna uhasama mkali baina yake na msanii mwenzake Diamond Platnumz. Madai hayo yaliibuka kwa mara ya kwanza wakati msanii Chidi Benz anahojiwa katika kituo cha Wasafi FM.

Soma Pia: Diamond, Rayvanny na Harmonize Waongoza Wanamuziki wa Bongo Waliotazamwa Zaidi YouTube Mwezi Agosti

Kwa mujibu wa Chidi Benz, tofauti baina ya wasanii hao wawili ulianza baada ya Diamond kuvichukua viatu vya Tunda Man bila idhini yake. Kwa wakati huo, Diamond alikuwa bado mchanga kimuziki huku Tunda Man akiwa jina kubwa sana katika muziki wa bongo.

Akizungumza na Wasafi TV katika mahojiano ya hivi karibuni, Tunda Man alikiri kuwa ni ukweli Diamond alivichukua viatu vyake. Ila aliongeza kwa haraka kuwa hana kinyongo na Diamond kama ilivyokuwa imedaiwa.

Alisema kuwa yeye hana ubaya na Diamond na hawezi zungumza lolote baya kwa Diamond haswaa ikizingatiwa hadhi na nafasi yake katika tasnia ya muziki.

Soma Pia: Diamond Platnumz Adokeza Ujio wa Tamasha Jipya ‘Swahili Festival’

Tunda Man vile vile alisimulia jinsi alikuwa na ukaribu na Diamond katika enzi za kale za bongo. Alifichua kuwa alimpigania sana kusudi yeye kuonekana kimuziki. Diamond aliwahi tokea katika video ya wimbo wa Tunda Man wa 'Starehe Gharama'.

"Baada ya miaka kumi sijalizungumzia hili suala. Sitaki kulizungumzia hilo suala. Maana nitagombana na mashabiki wangu, nitagombana na watu wangu, nitagombana na watu tofauti. Sitaki kuzungumzia hayo mambo. Kwa level aliyofikia Nasibu sitaki kuzungumzia mabaya kwa Nasibu," Tunda man alisema.

Aidha, Tunda man ni rafiki wa karibu wa msanii Alikiba ambaye ni mpinzani mkuu wa Diamond.

Leave your comment