Diamond Platnumz Adokeza Ujio wa Tamasha Jipya ‘Swahili Festival’

[Picha: The East African Feed]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi wa lebo ya WCB Diamond Platnumz amewasha tena moto kwenye tasnia ya muziki nchini Tanzania baada ya kutangaza ujio wa tamasha jipya lenye jina la ‘Swahili Festival’.

Mshindi huyo wa tuzo ya Afrimma amedokeza juu ya ujio wa tamasha hilo kupitia akaunti yake ya Instagram kwa kuchapisha picha nzuri yenye maneno "Swahili Fest" kisha kusindikiza na hashtag "#swahilination na kama kawaida ya Simba, hakuweka taarifa zaidi juu ya chapisho lake.

Soma Pia: Mbinu Alizotumia Diamond Platnumz Kufikisha Watazamaji Bilioni 1.5 Kwenye YouTube

Tangazo hilo limezua taharuki kubwa sana kutoka kwa wadau wa burudani nchini Tanzania kwa kuwa linakuja kipindi ambacho wengi wanasubiria ujio wa tamasha la Wasafi Festival ambalo hufanyika kila mwaka.

Ikumbukwe kuwa, Diamond Platnumz wiki chache nyuma alitangaza kuwa na ziara nchini Marekani ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu na anatarajiwa kutumbuiza kwenye maeneo miji na  majimbo tofauti tofauti nchini humo kama Washington DC, Atlanta, Seattle, Minneapolis, New York, Louisville, Arizona, Boston, Houston na Dallas.

Soma Pia: Diamond Aweka Rekodi Mpya YouTube Baada ya Kupata Watazamaji Bilioni Moja Nukta Tano

Tamasha hilo linaaendeleza msururu wa matamasha ambayo wasanii wa WCB wanatumbuiza kwani mathalan Zuchu alitumbuiza uwanja wa Amani Agosti 21 mwaka huu na siku chache zilizopita, alitetemesha jiji kutokana na onyesho lake yeye na Rayvanny pale Beach Kidimbwi.

Kufikia sasa, bado uongozi wa Wasafi haujatoa taarifa rasmi juu ya tamasha hilo

ila bila shaka mashabiki ni wengi ambao wanasubiria muongozo kutoka Wasafi.

Leave your comment