Beka Flavour Adai Kiki Zinaleta Ugumu Kwenye Mziki Tanzania

[Picha: Beka Flavour Facebook]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki wa bongo Beka Flavour amewaomba wasanii wa Tanzania kupunguza kiki na kuongeza bidii katika muziki. Beka flavour ambaye jina lake halisi ni Bakari Katuti anaamini kuwa kiki zimeongezeka bongo na kuathiri vibaya tasnia ya muziki.

Soma Pia: Beka Flavour Afichua Sababu Kuu Iliyofanya Yamoto Band Kuvunjika

Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni, Beka flavour alirejelea kauli yake aliyochapisha mtandaoni mapema mwakani kuwa kiki zimezuia wasanii chipukizi kupata mwangaza wanaostahili.

Aliongeza kuwa wapo wasanii wanaofanya muziki mzuri ila kazi zao zinafunikwa na kiki za wasanii wengine ambao wako na ufuasi mubwa mtandaoni.

Beka Flavour alilalamika kuwa wasanii chipukizi wamepuuziliwa mbali na hawapewi nafasi ya kung'aa licha ya kutia bidii katika nyimbo zao. Aliongeza kuwa yeye husikiliza kazi za wasanii ambao hawajatoka kusudi kujifunza mengi.

Soma Pia: Beka Flavour Akubaliana na Wazo la Kuirudisha Yamoto Band Pamoja

"Kweli namaanisha kuwa wapo watu siku izi hawasikilizi miziki. Wapo watu wako tayari kufuatilia mtu kwa sababu ya vitu zake anazofanya tofauti na muziki. Na wanamsapoti yaani kwa asilimia zote. Alafu mtu mwingine ambaye anatoa muziki kama muziki na mzuri, na wasimzingatie wala kumsapoti. Kwa hivyo inaleta ugumu," Beka Flavour alisema.

Msanii huyo alisema anatamani sana kama wasanii wa bongo wangejihusisha na muziki tu na wala si masuala mengine ya kuwapa umaarufu mtandaoni.

Katika taarifa aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram mwezi wa pili mwaka huu, Beka Flavour alidai kuwa muziki wa bongo utaelekea kufa iwapo kiki zitashamiri na kufuatiliwa sana kuliko muziki.

Katika taarifa hiyo, Beka Flavour pia aligusia suala la wasanii kuingiliana vibaya kusudi kuchafuana majina.

Leave your comment

Top stories

More News