Rich Mavoko Kuachia Wimbo Mpya ‘Ndo Mana’

[Picha: CitiMuzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Rich Mavoko yuko mbioni kuachia wimbo wake mpya uitwao ‘Ndio Maana’ ambao unatarajiwa kutoka siku moja kuanzia sasa.

Mkurugenzi huyo wa lebo ya Bilionea Kid alitoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram.

Read Also: Rich Mavoko Azungumzia Tofauti Baina yake na Diamond Platnumz

 "You all my people get ready for the smash hit… Its gonna be lit stay tuned in all digital platforms" aliandika msanii huyo.

Kwa wanaofuatilia nyendo za Rich Mavoko bila shaka hawatashangaa juu ya ujio wa wimbo huu kwani, kwa wiki kadhaa sasa Mavoko amekuwa akitembelea vyombo vya habari tofauti akifanya mahojiano.

Bila shaka, wengi walitegemea kuwa wimbo mpya kutoka kwa Bilionea Kid upo Jikoni.

Kwa sasa, Mavoko ambaye miaka michache nyuma alikuwa chini ya lebo ya WCB anatamba na wimbo wake wa ‘Nidonoe’ aliouachia mwezi Julai.

Read Also: Rich Mavoko Azungumzia Kufanya Kazi na Harmonize

‘Nidonoe’ ni wimbo uliopokelewa kwa mikono miwili na mashabiki wa muziki nchini Tanzania kutokana na kuwa na mashahiri mepesi. Kufikia sasa, wimbo huo umeshatazamwa takriban mara laki tisa sitini na nane kwenye mtandao wa YouTube.

Rich Mavoko ni mmoja wa wasanii wanaotoa ngoma zikifuatana mwaka huu. Inakisiwa kuwa msanii huyo anajitaidi ili kuwa miongoni mwa mastaa wakubwa Bongo, licha yay eye kuchukua likizo ya zaidi ya mwaka mmoja hapo mbeleni.

Leave your comment