Navy Kenzo Wadokeza Ujio wa Albamu Yao Mpya ‘Dread & Love’

[Picha: Citimuzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kundi la muziki kutokea nchini Tanzania Navy Kenzo wamedokeza kuwa wako jikoni kuandaa albamu yao mpya.

Leo kupitia ukurasa wao, kundi hilo ambalo limeundwa na Aika pamoja na mtayarishaji wa muziki Nahreel walichapisha picha ikiwaonesha wako pamoja na kuandika "Baby Dont tell them our secret Dread & Love album in the making."

Soma Pia: Navy Kenzo watoa Album Mpya

Aika ambaye ni mshiriki wa kundi hilo ambalo lilishinda tuzo ya Soundcity kama Kundi barani Afrika mwaka 2019 aliendeleza kudokeza juu ya ujio wa albamu hiyo kwa kuandika kwenye akaunti yake "I know you will love the Dread and Love Album its giving me all kinds of confidence."

‘Dread And Love’ album inategemewa kuwa albamu ya tatu kutoka kwa Navy Kenzo kwani Septemba mwaka 2020 kundi hilo lilitoa albamu yao ya ‘Story Of The African Mob’ ambayo ilishirikisha wasanii kama Nandy, Mzvee, Genius Genie, Tiggs da Arthur, King Promise, The Great Eddy and Mugeez.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Navy Kenzo Waachia Video Mpya ‘Nisogelee’

Mwaka 2017, kundi hilo liliachia albamu yake ya ‘Above In a Minute’ ambayo ilisheheni nyimbo kama ‘Lini’ waliomshirikisha Alikiba, ‘Bajaj’ waliomshirikisha Patoranking, ‘Done’ waliofanya na Mr Eazi na nyinginezo nyingi ambazo zilitikisa kiwanda cha Bongo Fleva.

Kwa sasa, Navy Kenzo wanatamba na wimbo wao wa ‘Nisogele’ ambao uliweza kusherehesha sana kwenye klabu pamoja sehemu mbalimbali za starehe hapa nchini Tanzania.

Kundi la Navy Kenzo lilianza mara baada ya kuvunjika kwa kundi la Pah One na hapo ndipo Aika na Nahreel wakatengeneza kundi hilo mwaka 2013 na wakatamba na nyimbo zao kama ‘Hold Me Back’, ‘Game’, ‘Chelewa’, ‘Kamatia Chini’ na nyinginezo nyingi ambazo zimetamba hapa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Leave your comment