Gigy Money Hatimaye Apanda Jukwaani Baada ya Marufuku Dhidi Yake Kukamilika

[Picha: Gigy Money Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu nchini Tanzania Gigy Money hatimaye ameweza kupanda jukwaani na kuwatumbuiza mshabiki wake baada ya kupigwa marufuku na BASATA.

Mapema mwaka huu, Gigy Money alipigwa marufuku ya kutotumbuiza au kupanda jukwaani nchini Tanzania. Marufuku hiyo ilitokana na Gigy Money kupanda jukwaani akiwa amevaa nguo zenye utata. BASATA ilimuadhibu Gigy Money kwa kuvaa nguo zisizofaa.

Soma Pia: Mkubwa Fella Afunguka Kuhusu Bendi Mpya ya New Yamoto Band

Msanii huyo alikatazwa kutotuimbuiza kwa muda wa miezi sita. Hata hivyo, si yeye tu ambaye aliadhibiwa kwani televisheni ya Wasafi TV iliyopeperusha tamasha alikotumbuiza Gigy Money pia aliadhibiwa. Wasafi TV hata hivyo baadaye ilisamehewa.

Gigy Money katika ujumbe aliouchapisha mtandoni alionekana mwingi wa furaha baada ya kupata fursa ya kutumbuiza katika tamasha la Zuchu Homecoming iliyofanyika wikendi.

Soma Pia: Harmonize Afichua Sababu Iliyomfanya Kuanzisha Lebo ya Konde Music Worldwide

Alikiri kuwa alikuwa amewakosa mashabiki wake kwa muda mrefu ila sasa alifurahi kuwa anaweza kurudi jukwaani tena.

"Kiukweli niliwamiss sana mashabiki zangu na pia @officialzuchu umeweza umewezaa tena @michaelwilliams.x Nakuja tunakikao haiwezi ikawa ivi jamani nilipendeza mno," chapisho la Gigy Money lilisomeka.

Hapo awali Gigy Money aliandika ujumbe wa malalamishi na kudai kuwa alikuwa bado anapokea adhabu ya marufuku licha ya muda wa miezi sita kuisha. Msanii huyo alisema kuwa maslahi yake yalikuwa magumu alipopigwa marufuku kwani hakuwa na kipato kingine kando na muziki.

Gigy Money ni mmoja wa wanamuziki wa kike wenye ushawishi mkubwa sana nchini Tanzania.

Leave your comment