Mkubwa Fella Afunguka Kuhusu Bendi Mpya ya New Yamoto Band

[Picha: Mkubwa Fella Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkubwa Fella ambaye ni mlezi wa vipaji vya muziki na pia muanzilishi wa bendi mbali mbali zilizotajika kama vile TMK Wanaume, amefunguka kuhusu bendi mpya iitwayo New Yamoto Bnad ambayo ameanzisha hivi karibuni.

Soma Pia: Beka Flavour Apongeza Mkubwa Fella kwa Kuanzisha New Yamoto Band

Fella amesifiwa na wadau wengi katika tasnia ya muziki kwa ujuzi wake wa kukuza wasanii ambao huishia kuwa majina makubwa sana. Miaka michache zilizopita, Mkubwa Fella alianzisha kundi la Yamoto Band ambalo lilipata umaarafu mkubwa sana ndani na nje ya Tanzania.

Bendi hiyo ambalo lilikuwa na wasanii wanne; Enock Bella, Aslay, Maromboso na Beka Flavour lilitamba sana na kupata mafanikio makubwa. Tofauti ziikuja zikaibuka baina ya wasanii hao na kuelekea kuvunjika kwa bendi.

Miaka michache baada ya bendi hiyo kuvunjika, Mkubwa Fella amelitambulisha kundi mpya ambalo ni New Yamoto Band. Kundi hili mpya limechukua mfumo wa kundi asili la Yamoto Band, kwana lina wasanii wanne pia ambao wanachipuka.

Soma Pia: Ujumbe wa Zuchu Kwa Mashabiki Baada ya Tamasha Lake Kupata Mafanikio

Katika ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Mkubwa Fella alisema kuwa anawatakia mema wasanii hao chipukizi na kuwaombea kuwa hao pia hawatavunjika kama vile kundi asili.

"Nafungua sanduku lengine la nyoka wapya. Sijui watanigonga nawao maana nikonao wengine huu mwaka wa nane wengine mwaka wa nne wengine mwaka mmoja sijui yupi ataanza kuwa google ila muhimu kumtanguliza Mungu na kumkabidhi vijana wako awa najalibu kuwapeleka mjini walinde lakini pia wasikutane na mashetani watu kuwa lubuni na kuwaacha njiani ameeeen inshallah lakini pia nawale wanao wasaidia kulalamika tuanze wote kuwajenga sio mwaka wamavuno," ujumbe wa Mkubwa Fella mtandaoni ulisomeka.

New Yamoto Band lilipata fursa ya kutumbuiza katika tamasha la Zuchu Homeconing lililofanyika Zanzibar.

Leave your comment