Beka Flavour Apongeza Mkubwa Fella kwa Kuanzisha New Yamoto Band

[Picha: Beka Flavour Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Bongo Beka Flavour amejitokeza na kumpongeza bosi wake wa zamani Mkubwa Fella kwa kuianzisha tena kundi la Yamoto Band upya. Yamoto Band ya kwanza ilianzishwa ikiwa na wasanii wanne chini ya usimamizi wa Mkubwa Fella.

Soma Pia: Nyimbo Mpya : Rayvanny Aungana na Whozu, Ntoshi Gazi Kuileta ‘Chawa’ [Video]

Wasanii hao wanne walikua Aslay, Beka Flavour, Mbosso pamoja na Enock Bella. Baada ya kundi hilo kupata mafanikio makubwa, liligawanyika huku kila msanii akienda zake na kuwa mwanamuziki huru.

Yamoto Band lilikuwa miongoni mwa makundi ya wanamuziki wanaopendwa sana si Tanzania tu bali Afrika mashariki. Kuvunjika kwake hivyo basi kulikuwa pigo kubwa wa mashabiki wa kundi hilo.

Soma Pia: Zuchu Amsifia Kidene na Kumkaribisha Kwenye Tamasha la Zuchu Homecoming

Miaka michache baada ya kuvinjika kwa Yamoto Band asili, Mkubwa Fella ameifufua tena jina la kundi hilo japo kwa kutumia wanachama tofauti. Kama vile alivyofanya mara ya kwanza ambapo aliwachukua wasanii chipukizi wenye talanta, Fella pia mara hii amechukua wasanii chipukizi na kuwaleta pamoja ili kuunda New Yamoto Band.

Beka Flavour alimpongeza Mkubwa Fella na kumwombea baraka kwa Mungu ili kundi hilo mpya pia liweze kupata mafanikio kama walivyopata hao.

"Haki yake anaweza kulitumia tu lile jina kama alivyolitumia kuwapa watu wengine ili waliendeleze kwa sababu Yamoto tena haipo. Kwa hivyo kawachukua vijana wengine kawatengeneza kama sisi alivyotutengeneza, kaamua kukwepa maneno mengi akaongeza New Yamoto Band. Iko sahihi mimi sioni ubaya. Anataka kuwasaidia wale wafanikiwe kama tulivyofanikiwa sisi. Na mimi namwombea Mungu sana," Beka Flavour alieleza.

Leave your comment