Hanscana Ajibu Madai ya Kuchukua Nafasi ya Kenny Pale Zoom Extra

[Picha: EATV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Director wa video za muziki nchini Tanzania Hanscana kwa mara ya kwanza amejitokeza kuelezea kufanya kazi na lebo ya Wasafi, kwa kile ambacho wengi wamekichukulia kama kuchukua nafasi ya Director Kenny.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa Bongo na Wasanii Diamond, Rayvanny, Zuchu na Ibraah

Hanscana kwa siku za hivi karibu ameonekana kuwa karibu sana Wasafi kwani ndiye aliyehusika kuandaa video ya Diamond Platnumz ‘Iyo’ pamoja na ‘Nyumba Ndogo’ ya Zuchu. Hanscana kuandaa video hizi ilishtua wengi kutokana na Kenny kuwa ndiye uhusika katika kutayarisha video za Wasafi kwa muda sasa.

Akizungumza kwenye kipindi cha Refresh, Hanscana ambaye hupendelea kuitwa Godfather aliweka wazi kuwa yeye bado anajisimamia mwenyewe kupitia Hanscana brand na wala hajachukua nafasi ya Kenny pale Zoom Extra.

"Mimi sifanyi kazi na Zoom production mimi ni Hanscana Brand mmiliki wa kampuni yangu na wateja wangu ni mtu yeyote ambaye anajihusisha na sanaa," alizungumza Hanscana.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz Aachia ‘Naanzaje’

Mazungumzo juu ya Hanscana kuunganisha kampuni yake ya Hanscana Brand na Zoom Extra yalishika kasi siku za hivi karibuni baada ya Director Kenny kutoa jina la Zoom Extra kwenye wasifu wake wa Instagram, hivyo kusababisha wengi kudhani kuwa hafanyi kazi na Wasafi japo yeye mwenyewe bado hajaweka bayana hatima yake.

Hanscana ni mojawapo ya watengeneza video za muziki maarufu sana nchini Tanzania kwani ameshafanya kazi na wasanii wakubwa nchini humo kama Diamond Platnumz, Harmonize, Marioo, Alikiba, Vanessa Mdee na wengineo wengi.

Kwa sasa watu wengi wana hamu ya kujua kama video inayofuata ya Diamond Platnumz, Zuchu au msanii yeyote wa Wasafi ataiongoza Hanscana kutokea Hanscana Brand au Director Kenny kutokea Zoom Extra.

Leave your comment