Ommy Dimpoz, Nandy Waashiria Ujio wa Collabo Mpya Baada ya Kuonekana Pamoja Studioni

[Picha: Music in Africa]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii kutokea nchini Tanzania Ommy Dimpoz amedokeza juu ya ujio wake mpya kwenye muziki baada ya kuonekana akiwa studio na Nandy.

Kupitia video fupi aliyochapisha Ommy Dimpoz kwenye akaunti yake ya Instagram, msanii huyo anaonekana akirekodi wimbo na msanii Nandy huku Mr LG akiwa kando ya wasanii hao.

Soma Pia: Ibraah Ajibu Madai ya Kununua Watazamaji wa Wimbo wake ‘Jipinde’ Kwenye YouTube

Video hiyo imezidi kuwaaminisha mashabiki kuwa huenda kuna jambo zuri linaandaliwa kutoka kwa wasanii hao. Hii itakuwa sio mara ya kwanza kwa Nandy na Ommy Dimpoz kufanya kazi pamoja kwani mwaka jana wasanii hao walishirikana kwenye wimbo wa ‘Kata’.

‘Kata’ ni wimbo uliopendwa sana na mashabiki na kufikia sasa ushatazamwa mara milioni tano kwenye mtandao wa YouTube. Kwa sasa, msanii Ommy Dimpoz anatamba na wimbo wa ‘Show Time’ alioshirikishwa na msanii Chege.

Soma Pia: Khadija Kopa, Jux na Wasanii Wengine Watakaotumbuiza Kwenye ‘Zuchu Homecoming’ [Orodha Rasmi]

Tangu mwaka huu uanze, Ommy Dimpoz hajatoa wimbo wowote rasmi tangu alipotoa Amapiano ya ‘Dede’ aliomshirikisha DJ Tira, Dladla na Prince Bulo Desemba mwaka jana.

Kwa upande mwingine, Nandy bado anaendelea kutikisa na wimbo wake wa ‘Nimekuzoea’ kutoka kwenye EP yake ya ‘Taste’.

 Siku chache zilizopita kupitia akaunti yake ya Instagram, Nandy alidokeza ujio wa video ya ‘Yuda’ hivi karibuni. Kando na Nandy, Ommy Dimpoz ameshawahi kushirikisha wasanii wengine wengi kwenye nyimbo zake kama J Martins, Alikiba, Vanessa Mdee na Seyi Shay kutokea nchini Nigeria.

Leave your comment