Tunda Man Amshukuru Alikiba Kwa Kusimama Naye Kimuziki

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pakua Ngoma Zake tunda Man Bure Kwenye Mdundo

Msanii Tunda Man ambaye ni mmoja wa wanamuziki wakongwe zaidi kwenye tasnia ya muziki ya Tanzania amemshukuru Alikiba kwa kusimama naye katika safari yake ndefu ya muziki. 

Soma Pia: Khadija Kopa, Jux na Wasanii Wengine Watakaotumbuiza Kwenye ‘Zuchu Homecoming’ [Orodha Rasmi]

Kupitia chapisho kwenye ukurasa wake wa Instagram, Tunda Man alifunguka kuwa Alikiba amesimama naye kwenye muziki licha ya yeye kupitia changamoto chungu nzima. Msanii huyo alisema kuwa wapo wanaojaribu kumkatisha tamaa katika muziki, ila alisisitiza kuwa kamwe hatoacha muziki.

Msanii huyo pia aliwashakuru wasanii wengine wote waliomsaidia kwa njia moja au nyingine, lakini hakuwataja kwa majina.

Soma Pia: Baba Levo Afichua Sababu ya Zuchu Kukataa Mkataba wa Mamilioni ya Pesa

Tunda Man ambaye kwa sasa anatamba sana na ngoma yake ya True Love alituma ujumbe huo huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.

“Leo nimezaliwa Ahsante Mama Tunda Ahsante ALLAH mwingi wa Rehema....Mziki ndio kazi yangu wapo wanaonikatisha tamaaa wapo wanaonipongeza yote kwa yote nasema Ahsante MUNGU... Thanx ndugu yangu @officialalikiba kwa kuwa na mimi bega kwa bega kwenye shida na raha thanx wasaniii wenzangu wote kwa ushirikiano wenu kwangu ...Happybirthday to me!" ujumbe wa Tunda Man kwenye mtandao ulisomeka.

Leave your comment