Baba Levo Afichua Sababu ya Zuchu Kukataa Mkataba wa Mamilioni ya Pesa

[Picha: Baba Levo Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Baba Levo amefichua kuwa Zuchu alikataa dili ambayo ingempea mamilioni ya pesa. Kulingana na taarifa ambayo Baba Levo alitoa, dili hiyo ilihusiana na utangazaji wa pombe. Baba Levo alieleza kuwa Zuchu alikataa kutangaza pombe au kujihusisha na utangazaji wa pombe kwa sababu ya imani na dini yake ya kiislamu.

Soma Pia: Amber Lulu Alalamika Kutoshabikiwa Kama Wasanii Walio Kwenye Lebo Tajika Tanzania

Japo Babe Levo hakufichua maelezo zaidi, aliiendelea kwa kuibua maswali kuhusiana na maadili yaliopo kwenye wimbo wa Zuchu wa Nyumba Ndogo. Msanii huyo ambaye alikuwa akizungumza na kituo cha Wasafi FM, alisema kuwa uamuzi wa Zuchu wa hapo awali kuhusiana na utangazaji, unatofautiana na mada iliuopo kwenye wimbo wake.

 "Zuchu amekataa dili ya milioni mia nne kwa sababu ya msimamo kwamba hawezi kutangaza pombe, sawa, msimamo wake wa ki imani. Alafu baada ya hapo akaenda kufumua goma linaloitwa Nyumba Ndogo akimchamba nyumba kubwa," Baba Levo alisema.

Soma Pia: Rosa Ree Kuwakutanisha Frida Amani, Chemical Ndani ya Ngoma Moja

Zuchu hapo awali alipoulizwa kuhusu uwepo wa utata kutokana na wimbo wake wa Nyumba Ndogo, alisema kuwa yeye hakuwa anachochea yeyote bali lengo lake lilikuwa kuburudisha tu.

Alisisitiza kuwa hakuwa na nia mbaya wakati akiunda hiyo ngoma na hivyo basi mashabiki waburudike tu na wala wasiichambue ngoma hiyo vibaya.

Zuchu ni mmoja wa wasanii wa bongo wanaoheshimiwa kwa maadili mema nan i mmoja wawasanii wasio na utata wala kiki.

Leave your comment