Zuchu Aeleza Jinsi Familia Yake Ilivyomkuza Kimuziki

[Picha: 3 Neel]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Zuchu amefunguka kuhusu mchango ambao familia yake ilikua nayo katika kukuuza taaluma yake ya muziki. Zuchu kwa sasa ni miongoni mwa wasanii wa bongo wanaoshabikiwa sana Afrika Mashariki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu Aachia ‘Yalaaaa’

Zuchu aliwashangaza wengi kutokana na mafanikio yake makubwa kimuziki ndani ya muda mfupi sana. Wasichokijua wengi ni safari yake ndefu katika muziki. Safari hiyo ilianza akiwa mchanga sana.

Kipaji chake kilikuzwa na mamake Khadija Kopa ambaye pia ni jina kubwa la kuheshimika ikija kwenye tasnia ya muziki ya Tanzania. Zuchu amefunguka kupitia chapisho aliloliweka mtandaoni kuhusiana na jinsi familia yake ilichangia katika kunawiri kwake kimuziki.

Soma Pia: Zuchu Amsifia Kidene na Kumkaribisha Kwenye Tamasha la Zuchu Homecoming

Msanii huyo ambaye kwa sasa amesainiwa na lebo ya WCB alisema kuwa ndoto yake ya kuimba ilianzia nyumbani kwao. Aliongezea kuwa alishikwa mkono na kuelekezwa vizuri katika safiri ya sanaa ya muziki.

Aidha, Zuchu alichapisha video iliyoashiria kuwa mamake ndiye alimfunza mengi haswaa ikija kwa muziki.

"Ndoto yangu ilianzia nyumbani, nikashikwa mkono na kuoneshwa njia. Njia ambayo imetengenezwa na watu wanaoniamini na kupokelewa nanyi .Njia hii kuipita pekupeku sio rahisi lakini Nimejidhatiti kuipita na kukabiliana nayo .Ninayoyaota ni makubwa na yananiogopesha lakini kuwaangusha watu walioniamini ni kujiangusha mimi hivyo basi wendo ni uleule kufanya ,na nikifeli siachi nitafanya tena na tena na tena mpaka nifike," ujumbe wa Zuchu mtandaoni ulisomeka.

Kwa sasa, Zuchu anatamba na ngoma yake mpya ya 'Yalaaaa'.

Leave your comment