AY Aeleza Alivyoshirikiana na Mimi Mars Kwenye ‘Stakaba’

[Picha: Afro Charts]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Siku chache zilizopita msanii AY alitoa wimbo wake unaoitwa ‘Stakaba’ akimshirikisha mwanadada Mimi Mars kutokea lebo ya Mdee Music.

‘Stakaba’ umepokelewa na kufanya vizuri nchini Tanzania na eneo la Afrika Mashariki. Kwenye mahojiano yake na mtangazaji Lil Ommy, AY aliweka wazi kuwa yeye ndiye alimuelekeza Mimi Mars jinsi ya kuimba kiitikio cha wimbo huo na alifanya hivyo kwa njia ya simu.

"Mimi Mars nimemuelekeza kwenye simu kuimba mara ya kwanza nilikuwa nae mara ya pili alivyofanya hii ya hapa ya mwisho (kurekodi) nilimelekeza kwenye simu," alifafanua msanii huyo.

Soma Pia: AY Ataka Tuzo za Muziki Zirudi Tanzania

Wimbo wa ‘Stakaba’ imetayarishwa na Daxo Chali na tangu kutoka kwake umekuwa ni wimbo pendwa sana hapa Tanzania na mpaka sasa kwenye mtandao wa YouTube, video ya wimbo huo imeshatazamwa mara laki moja na elfu nne.

Aidha, miaka kadhaa nyuma AY alishawahi kufanya kazi na Vanessa Mdee ambaye ni dada yake Mimi Mars kwenye wimbo wa ‘Money’.  Kwenye mahojiano hayo, AY alieleza kuwa yeye na Vanessa ni marafiki tangu kitambo kabla hata Vanessa hajachukua likizo ya muziki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Mpya Zilizoachiwa na Rayvanny, Jux, Marioo na AY

"Tangu Vanessa yuko hapa tulikuwa tunahang pamoja tangu B Hits enzi zile anaanza (Vanessa) kurekodi na hata nshafanya nae nyimbo mbili nyingine nyuma kabla ya hiyo ‘Money’,” alidokeza AY.

AY ni mojawapo ya wasanii wanafanya vizuri sana nchini Tanzania. Safari yake ya muziki ilianza mwaka 1996 kwenye kundi la S.O.G na ilipofika 2002 alianza kufanya muziki kama msanii huru na tangu hapo anasifikia kwa kutoa nyimbo zilizotamba sana Tanzania kama ‘Habari Ndio Hiyo’, ‘Zigo Remix’, ‘Danhella’ na nyinginezo nyingi.

https://www.youtube.com/watch?v=qvtiVJ5fWbY

Leave your comment