Zuchu Adhibitisha Ujio wa Ngoma Wake Mpya Hivi Karibuni

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu kutoka mkoa wa Zanzibar Zuchu kwa sasa amekuwa mada kuu baina wa wadau mbali mbali katika tasnia ya muziki ya Tanzania. Hii inatokana na mambo tofauti mojawapo ikiwa tamasha lake la Zuchu Homecoming na pia mafanikio ambayo ngoma zake zimekuwa zikipata.

Soma Pia: Zuchu Amsifia Kidene na Kumkaribisha Kwenye Tamasha la Zuchu Homecoming

Licha ya umaarufu na mafanikio ambayo Zuchu amepata, hajapunguza kasi bali ameongeza haswaa ikija katika kuachia miziki. Mnamo tarehe 15 mwezi huu Zuchu alidhibitisha uwepo wa nyimbo yake mpya.

Zuchu hata hivyo hakufichua maelezo mengi kuhusiana na wimbo hiyo bali alichapisha tu video ambayo ilimuonyesha mamake Khadija Kopa akiburudika na wimbo hiyo.

Msanii huyo pia hakusema tarehe ambayo ataachia ngoma hiyo na hivyo basi kuwaacha mashabiki wake na hamu. Zuchu katika chapisho lake mtandaoni alisema kuwa alikuwa ameisikilizisha familia yake ngoma hiyo mpya ambayo imetayarishwa na S2kizzy.

Soma Pia: Zuchu Aibua Hisia Baada ya Kuimba Wimbo wa Sabaha Salum ‘Mithili yako Hapana’ 

Tangazo la Zuchu la uwepo wa ngoma yake mpya linakuja muda mfupi tu baada ya yeye kuachia ngoma ya ‘Nyumba Ndogo’ ambayo ilivuma sana mtandaoni na kumpa mafanikio makubwa.

"Familia wamenivamia kwa zombie @s2kizzy Nimewasikilizisha Goma Letu Jipya Basi Kama Mnavyoowaona hapo," Chapisho la Zuchu katika ukurasa wake wa Instragram ulisomeka.

Hapo awali, Zuchu pia alikuwa ametangaza kuwa anahitaji ulinzi zaidi kabla ya kuachia ngoma yake. Alisema kuwa ngoma hiyo huenda ikahatarisha maisha yake ila hakueleza sababu kamili ya hofu yake.

 

Leave your comment