Zuchu Aibua Hisia Baada ya Kuimba Wimbo wa Sabaha Salum ‘Mithili yako Hapana’

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika Zuchu amevutia mashabiki wengi kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuchapisha video iliyomwonyesha akiimba wimbo wa ‘Mithili yako Hapana’ ulioachiwa na msanii Sabaha Salum.

Sabaha Salum ni mmoja wa wasanii wakongwe zaidi na pia wanaoheshimika katika tasnia ya muziki Tanzania.

Soma Pia: Zuchu Afichua sababu ya Maua Sama, Nandy kukosa Kwenye Tamasha la Zuchu Homecoming

Yeye huimba kwa mtindo wa taarab na nyimbo zake huvutia wengi sana. Katika chapisho lake mtandaoni, Zuchu alifichua kuwa alipenda nyimbo za Sabaha Salum tangu enzi zake akiwa mchanga kimuziki.

Zuchu aliongezea kuwa alitumia nyimbo hizo kujifunza kuimba. Kulingana na Zuchu, Sabaha Salum ni kama mama yake kimuziki. Aidha, Zuchu alielezea furaha aliyokuwa nayo kwani Sabaha Salum atakuwepo kwenye tamasha lake la Zuchu Homecoming mnamo tarehe 21 mwezi huu katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

Soma Pia: Zuchu Ajibu Madai ya Uhasama Baina Yake na Queen Darleen

Zuchu aliwaelekeza mashabiki wake wachague nyimbo moja amabayo wangependa kumsikia akiimba kwa ushirikiano na Sabaha Salum.

"Moja kati ya nyimbo nazozipenda sana kutoka kwa @sabaha_salum. Nimejifunzia kuimba kwenye nyimbo zake nafurahi mno leo napata bahati ya kushare nae stage moja ...Chagueni wimbo wake mmoja niimbe nae siku ya Zuchu Homecoming," ujumbe wa Zuchu ulisoma.

Sabaha Salum kwa upande wake alichapisha ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumsifia Zuchu kama mwenye talanta ya kuvutia mno.

"Mwanangu kipenzi @officialzuchu mrith wa @officialkhadijakopa mashaallah mwenye kipaji cha kutoa nyoka pangoni," Salum aliandika.

Tazzama Video HAPA.

Leave your comment