Zuchu Aelezea Changamoto Anazopitia Katika Kuandaa Tamasha la Zuchu Homecoming

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Zuchu kwa sasa ni gumzo miongoni mwa wadau mbali mbali katika tasnia ya burudani ya Tanzania kutoka na tamasha lake la Zuchu Homecoming litakalo fanyika tarehe 21 mwezi huu.

Wadau wengi wanachambua maandalizi ya tamasha hilo na uwezekano wa mafanikio yake. Kikubwa sana ambacho wengi wanatarajia kuona ni iwapo Zuchu atafikia kiwango kilichoekwa na wasanii wenzake wa kike haswaa Nandy ambaye amefanya tamasha mingi sana.

Soma Pia: Zuchu Afichua Siri Inayoleta Mafanikio Makubwa Kwa Wasanii wa WCB

Zuchu amejitokeza na kufunguka kuwa anapitia changamoto chungu nzima katika maandalizi kwani hili ndilo tamasha la kwanza ambalo anajisimamia kama mwanamuziki. Tatizo la kwanza ni kuwa yeye bado ni mchanga katika sekta hii ya kujiandalia tamasha na hivyo basi kuna mengi ambayo hayajui.

Soma Pia: Zuchu Atoa Ushauri kwa Wasanii Chipukizi Wanaotaka Kujikuza Kimuziki

Zuchu, hata hivyo, alieleza kuwa anafanya kazi pamoja na wadau mbali mbali wanaomsaidia. Tatizo lingine ni kuwa baadhi ya wasanii ambao walioalikwa kuburudisha kwenye tamasha lake hawangeweza kutikia mwaliko kwani walikua na shughuli nyingine za kikazi.

"Nikikuelezea ma usiku mangapi sijalala huenda usiniamini kwa hofu tu... Lakini jana usiku sijalala, nimepata usingizi mchache sana kuanzia saa kumi hivi. Lakini niseme ni moja kati ya changamoto. Mimi nimechoka kuwa wa kawaida kila siku hatua zangu za numbers pia nataka ziende kwa ukubwa ambao nautazamia mimi," Zuchu alisema.

Zuchu ni mmoja wa wasanii wa kike wanaovuma sana kwa sasa nchini Tanzania. Yeye pia ni msanii ambaye ameandikisha mafanikio makubwa sana ndani ya muda mfupi tangu yeye kutambulishwa rasmi kama msanii wa WCB takriban mwaka mmoja uliopita.

Leave your comment