Harmonize Kuachia Ngoma Nyingine Baada ya Mang'Dakiwe Kupata Mafanikio Makubwa

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Harmonize ametangaza kuwa ataachia ngoma nyingine hivi karibuni kabla ya kuileta albamu yake ambayo imetarajiwa kwa hamu sana.

Tangazo hilo linakuja muda mfupi tu baada ya Harmonize kuachia ngoma kwa mtindo wa Amapiano. Ngoma hiyo inayoitwa Mang'Dakiwa ni remix na wasanii wa Afrika Kusini DJ Obza pamoja na Leon Lee wameshirikishwa.

Soma Pia: Harmonize Atangaza Kuachia Wimbo Mpya Wenye Jina ‘Mang'dakiwe’ Remix Wiki Hii

Ni muhimu kutaja kuwa ngoma asili ilifanyiwa na wasanii hao wawili DJ Obza na Leon Lee na ilipata mafanikio makubwa pia. Remix yake Harmonize imepokelewa vyema na mashabiki na kufikia sasa imeshapata watazamaji milioni moja na nusu kwenye mtandao wa YouTube.

Katika tangazo lake, Harmonize alionekana mwenye furaha na jinsi ngoma hiyo imepokelewa.

Aidha, kwenye chapisho hilo, msanii huyo aliambatanisha picha ambayo ilionyesha Mang'Dakiwe ikiwa miongoni mwa nyimbo zinazovuma zaidi nchini Tanzania. Harmonize, hata hivyo hakufichua tarehe kamili atakayoachia ngoma yake ya mwisho kabla ya albamu.

Soma Pia: Harmonize Afafanua Dhamira ya Kuachia wimbo wa ‘Sorry’

"I’m extra ready for my last song b4 the album who is ready?" ujumbe wa Harmonize aliyouchapisha kwenye mtandao wa Instagram ulisoma.

Harmonize hivi karibuni ameonekana kuachia ngoma mfululizo pasi na kupumzika. Hii huwenda ikatokana na ushindani uliopo kwenye tasnia ya muziki ya Tanzania, ambako kila msanii anajitahidi kubakia juu ya chati za muziki. Hapo awali, Harmonize alitoa wimbo wa ‘Sandakalawe’ ambayo pia ilifanya vizuri sana.

Leave your comment