Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Harmonize, Alikiba na Rich Mavoko Wiki Hii

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wiki ya mwisho ya Mwezi Julai imeshawadia na wasanii kama Harmonize, Alikiba, Rich Mavoko na wengineo wameamua kuipamba wiki hii kwa kutoa ngoma nzuri na zinazovutia wasikilizaji. Zifuatazo ni nyimbo tano mpya zilizotoka wiki hii:

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Tano 5 Zinazotamba YouTube Tanzania Wiki Hii

Mang'dakiwe Remix - DJ Obza ft Harmonize & Leon Lee

Msanii Harmonize kwa mara nyingine ameonesha kwamba yeye ni kiboko kwenye muziki wa Amapiano baada ya kuachia wimbo huu Julai 23 akiwa na DJ Obza na Leon Lee. Kwenye wimbo huu Harmonize ameonesha ni kwa namna gani alivyo akiwa ameshalewa pombe. Tangu remix ya wimbo huu itoke, umekuwa ni wimbo maarufu sana kwenye bar na sehemu mbalimbali za starehe. Kufikia sasa wimbo huu umeshatazamwa mara zaidi ya laki tano kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=h3eb4fYvk1U

Jealous - Alikiba

Kutokea Kings Music, msanii Alikiba Julai 22 alitoa wimbo wake uitwao ‘Jealous’ akimshirikisha Mayorkun kutokea Nigeria. Wimbo wa ‘Jealous’ umepata mapokezi makubwa sana na watu tofauti tofauti ikiwemo Baba Levo ambaye wamesifia wimbo huo uliotayarishwa na Yogo Beats. Kufikia sasa wimbo huu umetazamwa mara zaidi ya milioni moja kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=S1DQA8peH7M

Nidonoe - Rich Mavoko

Bilionea Kid ameendelea kuonesha ubabe wake kwenye muziki wa Bongo Fleva baada ya wiki hii kuachia wimbo wake mpya uitwao ‘Nidonoe’. Video ya wimbo huu ilitoka Julai 23 mwaka huu huku video ikiongozwa na Kmane na kufikia sasa wimbo huu umeshatazamwa mara laki tatu na elfu tisa kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=6ZGEa4LNllI

Kwani Unaogopa - Nay wa Mitego

Baada ya wimbo wake wa ‘Hawakatai’ kufanya vizuri, Ney wa Mitego amekuja kivingine na ‘Kwani Unaogopa’. Kupitia wimbo huu, Ney ameongelea mambo mengi yanayogusa jamii kama uongo, uzinzi, chuki na ulevi. ‘Hawakatai’ imetayarishwa na True name huku maandalizi ya mwisho yamefanywa na Awesome na kufikia sasa imeshatazamwa na watu tisini na tatu elfu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=kMxObUSyM2I

Simba Tunajidai – Tundaman

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii Tundaman mara kwa mara huweka wazi mapenzi aliyonayo na kupitia wimbo huu ‘Simba Tunajidai’, amezidi kuonesha ni namnna gani anaipenda timu hiyo. Kwenye wimbo huu, Tundaman ameonesha furaha yake ya kuwa mwanasimba vilevile amewahasa mashabiki wa simba kutembea kifua mbele kwani wana timu bora.

https://www.youtube.com/watch?v=TaIJhrReTvk

Leave your comment