Otile Brown Atangaza ujio wa Kolabo na Darassa

[Picha: Otile Brown Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Ushirikiano baina ya wasanii wa Kenya na wale wa bongo unazidi kunoga. Msanii kutoka Kenya Otile Brown ni mmoja wa wasanii wa Kenya ambaye amepata umaarufu sana nchini Tanzania baada ya kushirikiana na wasanii wa huko. Msanii huyo ametoa kolabo na waimbaji wa Tanzania kama vile Alikiba na Jux.

Soma pia:Babalevo Asisimua Mashabiki kwa Kusifia Ngoma Mpya Ya Alikiba 'Jealous'

Mwimbaji huyo  wa ‘Dusuma’, Otile Brown alitangaza kuwa yupo studioni akishughulikia wimbo wake mpya kwa ushirikiano na mwanamuziki wa kutoka kutoka Tanzania Darassa. Tangazo hilo liliwavutia mashabiki wengi ambao walionekana kupokea ujumbe huo kwa furaha.

Otile Brown katika chapisho lake kwenye ukurasa wa Instagram, aliambatisha ujumbe huo pamoja na picha ambazo zilimuonyesha akiwa pamoja na Darassa.

Picha hizo zinaaminika kuchukuliwa wakati wa kurekodi video ya wimbo wao wa pamoja. Aidha Otile Brown alidokeza kuwa kuna uwezekona kuwa ngoma hiyo itadondoshwa wiki lijalo.

Darassa anapendwa sana kutoka na uwezo wake wa kurap au ukipenda kufoka. Otile Brown kwa upande wake anafahamika sana kwa kuimba nyimbo za mahaba. Tofauti na Darassa, nyimbo mingi za Otile Brown huwa na kasi ya chini ili kuletea hisia ya mahaba.

Hivyo basi, mashabiki wengi wana hamu sana kusikiliza ngoma hiyo inayopikwa na Otile Brown pamoja na Darassa.

Kando na Darassa, wasanii wengine tajika waliowahi kufanya kolabo na wasanii wa Kenya ni pamoja na Rayvanny na Mbosso.

Leave your comment