Nyimbo Mpya: Rich Mavoko Aachia Wimbo Mpya 'Nidonoe'[Video]

[Picha: Rich Mavoko Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Zikiwa zimeshatimia siku tano tangu atoe audio ya wimbo wa wimbo wa "Nidonoe" hatimaye msanii Rich Mavoko amekonga hisia za mashabiki zake baada ya kuachia video ya wimbo huo. Video ya "Nidonoe" imeongozwa na Director kutokea nchini Zimbabwe aitwae K Mane ambae pia ameshafanya kazi na wasanii kama Barakah The Prince na Linex kwenye wimbo wa Ndinewe Remix. 

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba, Mayorkun Waachia Wimbo Mpya 'Jealous'

"Nidonoe" ni video iliyosheheni stori nzuri ambapo inamuonesha msanii Rich Mavoko akiwa ametekwa na kufungwa kwenye kiti huku mabinti warembo wanaonekana wakicheza kwa namna ya mitego mbele yake wazo ambalo pia msanii Rema kutokea nchini Nigeria alishawahi kutumia kwenye video yake iitwayo "Lady" iliyotoka Novemba 11 2019.

Pamoja na wimbo huu kuwa wa kuchezeka lakini msanii Rich Mavoko ameonekana kutulia huku muda mwingi akiwaachia mabinti wanaopamba video hiyo kucheza dansi. 

Soma Pia: Video 5 Zilizo na Watazamaji Wengi Zaidi YouTube Tanzania

Mara baada ya video hii kuchapishwa kwenye akaunti ya Rich Mavoko huko Youtube watu takribani 1,000 walipenda video hii huku maoni ya wadau wengi yakiwa ni chanya. 

Mchangiaji mmoja aliandika " Hii video ni kama movie tu" huku mchangiaji mwengine alionesha ni kwa namna gani anamkubali Rich Mavoko kwa kuandika "Nimeanza kukuelewa tena mzee baba ngoma kali sana. Safi sana tuendelee kujitafuta" 

Ikumbukwe kuwa mwezi Agosti mwaka jana msanii Rich Mavoko aliachia Ep yake inayoitwa "Mini Tape" iliyosheheni nyimbo saba na ni nyimbo nne tu kwenye EP hiyo ndio ambazo zimefanyiwa video huku Video ya "Nidonoe" ikiwa ni ya pili kwa Rich Mavoko kwa mwaka 2021. 

Kufikia sasa video ya "Nidokoe" imeshatazamwa takriban mara 11,000 kwenye mtandao wa Youtube. 

https://www.youtube.com/watch?v=6ZGEa4LNllI&ab_channel=BillioneaKid

Leave your comment