Sarah Amjibu Harmonize baada ya kuachia Wimbo Wa kuomba radhi 'Sorry'

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Siku zote sanaa ndio njia bora zaidi ya msanii kuelezea hisia zake. Wasanii wengi hutumia ufundi na ujuzi wao katika sanaa na kuwapasha mashabiki wao kuhusu hali tofauti wanazopitia katika maisha yao halisi. Baadhi ya wasanii wakubwa waliotumia sanaa ya muziki kuelezea hisia zao ni pamoja na Rayvanny na Diamond Platnumz.

Kwa sasa msanii tajika kutoka Tanzania Harmonize anavuma sana mtandaoni baada ya yeye kumwaga hisia nzito katika wimbo alioachia kwa jina la Sorry. Katika wimbo huo, Harmonize kwa mara ya kwanza alinyenyekea na kumwomba mpenzi wake wa zamani msamaha.

Soma pia: Nyimbo Mpya: Alikiba, Mayorkun Waachia Wimbo Mpya 'Jealous'

Harmonize kwenye wimbo huo alifuchua kwamba yeye ndiye alikuwa chanzo cha uhusiano wake na Sarah kuporomoka. Wawili hao walikuwa wamechumbiana kwa muda wa miaka minne kabla ya kuachana. Kwa wakati ambao walikuwa pamoja, ilikuwa nadra sana kusikia Harmonize akitajwa katika kashfa za mapenzi.

Sarah kwa upande wake amejitokeza na kumpa Harmonize jibu kupitia mtandao wa Instagram. Katika chapisho lilowekwa mtandaoni, Sarah alikiri kuwa ni jambo nzuri mtu kuomba msamaha baada ya kukosa.

"It is important to apologize after a big mistake (Ni vyema kuomba msamaha baada ya kosa kubwa)," ujumbe wa Sarah ulisoma.

Sarah hata hivyo hakutanganza msimamo wake au kusema wazi iwapo alikuwa amemsamea Harmonize au la.

Harmonize amesifiwa mno kwa kuwa mwingi mwenye busara katika ngoma yake mpya.

Leave your comment