Harmonize Amhimiza Korede Bello Kufanya Kolabo na Hamisa Mobetto

[Picha: Hamissa Mobeto Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi mkuu wa Konde Music Worldwide Harmonize amemshauri msanii Korede Bello kutoka Nigeria kufanya kolabo na Hamisa Mobetto kutoka Tanzania.

Harmonize katika mawasiliano yake na Korede Bello kupitia mtandao wa Instagram, alimisfia Hamisa Mobetto kama msanii wa kike anayevuma kwa sasa nchini Tanzania. Mawasiliano baina ya wawili hao yalianza baada ya Korede Bello kumpongeza Harmonize kwa wimbo wake aliyoachia hivi karibuni.

Soma Pia: Harmonize Awapongeza Nandy, Hamisa Mobetto na Anjella Kwa Kuachia Ngoma Zinazovuma

Wimbo wa Harmonize iliyopewa jina la Sorry imevutia wadau mbali mbali katika tasnia ya muziki huku wengi wao wakikubaliana kuwa kweli ni wimbo mzuri sana. Majibu ya Korede Bello kwenye ombi la Harmonize bado hayajajulikana.

Hivyo basi mashabiki wamengoja kwa hamu sana kuona iwapo Hamisa ataingia studioni na Korede Bello kuandaa wimbo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Mpya za Zuchu, Nandy na Anjella Zinazovuma Bongo Wiki Hii

"Make sure you make a song with Hamisa G she is too good here number one chick in the game no cap," Harmonize alisema.

Ujumbe wa Harmonize unakuja mda mfupi baada ya Harmonize kuwamiminia sifa wasanii Anjella, Nandy na Hamisa Mobetto. Nyimbo za wasanii hao watatu zilichukua nafasi tatu za kwanza kwenye mtandao wa YouTube. Kulingana na Harmonize, haikuwa historia tu bali pia habari njema kuwaona wasanii wa kike wakijizatiti na hata kuwapiku wenzao wa kiume.

"History imeandikwa tangu muziki uanze haijawahi tokea nyimbo (3) za wasanii wa kike wote kutoka hapa Tanzania zikafwatana kwenye trend mtandao wa Youtube kama hivyo zinavyo onekana ...!!!! Hongeleni sanaa oyaaaa wameamua  licha ya makelele yetu yote,"  Harmonize aliandika katika ukurasa wake wa Instagram.

Leave your comment