Rayvanny Kuachia Ngoma Mpya Baada ya ‘Jennifer Remix Kupata Mafanikio

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rayvanny amesafiri kwenda Zimbabwe ambako anatarajiwa kufanya kazi kwenye mradi wa muziki na msanii anayefahamika kama Rockford 'Roki' Josphats.

Ripoti zinaonyesha kuwa Rayvanny atakuwa akifanya kazi ya remix kwa moja ya nyimbo za Rockford ambayo bado haijajulikana.

Soma Pia: Zuchu ‘Sukari’ na Video Zingine za Wasanii wa Kike Bongo Zilizotazamwa Zaidi YouTube

Rockford 'Roki' Josphats ni miongoni mwa wanamuziki wanaotamba sana katika tasnia ya Burudani ya Zimbabwe. Amesainiwa chini ya lebo ya rekodi ya Passion Java ambayo inamilikiwa na Prophet Passion Java.

Prophet Passion Java ni rafiki wa karibu wa Rayvanny na anaonekana ndiye aliyesababisha  safari ya Rayvanny kwenda Zimbambwe. Passion Java alikuwepo wakati wa uzinduzi rasmi wa lebo ya rekodi ya Next Level ambayo inamilikiwa na Rayvanny.

Soma Pia: Zuchu Atangaza Ujio wa Tamasha la ‘Zuchu Homecoming’ Mwezi Ujao Zanzibar

Wakati wa uzinduzi, alitambulishwa kama rafiki wa karibu wa Rayvanny. Kwa upande mwingine, Rayvanny amekaa kimya kuhusu ziara yake Harare na bado hajafafanua maelezo ya wimbo ambao watafanya remix.

Hii inakuja muda mfupi tu baada ya Rayvanny kumaliza ushirikiano wake na mwanamuziki wa Nigeria Guchi kwenye wimbo wa ‘Jennifer Remix’.

Jennifer Remix imepokelewa vizuri na imepata watazamaji wengi ndani ya muda mfupi. Inaonekana kuwa idadi nzuri ya wanamuziki wa Kitanzania wanafanya kazi ya remix kwa nyimbo mbali mbali. Wanamuziki wengine ambao pia wametangaza kuwa wanaandaa remix ni Anjella na Harmonize.

Leave your comment