Frida Aweka Wazi Sababu ya Kumshirikisha Mimi Mars Kwenye ‘Imoo’

[Picha: Biggest Kaka]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Frida Amani ameeleza kuwa alimshirika Mimi Mars kwenye wimbo wake mpya uitwao ‘Imoo’ kwa kuwa ndiye msani aliyepata mda wa kufanya kazi naye kwenye ngoma hio.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Aslay Aachia Ngoma Mpya ‘Shangingi Mtoto’

Frida Amani akizungumza katika mahojiano kwenye kipindi cha XXL, alieleza kuwa alikuwa amewafikiria wasanii wengi sana kuwashirikisha kwenye wimbo wake ila hawakupata muda.

"Walikuja watu wengi kimawazo kiukweli lakini at the end of the day kwa sababu mambo ni mengi wakashindwa kuingia ikabidi aingie Mimi mars whichi ameua sana and I respect her" alisema msanii huyo kwenye mahojiano hayo.

Soma Pia: Zuchari ‘Sukari’ na Video Zingine za Wasanii wa Kike Bongo Zilizotazmwa Zaidi YouTube

Frida pia aliweka wazi kuwa msanii na mtayarishaji muziki Quick Rocca kutokea Switch Records ndiye aliyependekeza wimbo huo kuitwa ‘Imoo’. Sambamba na hilo, Frida alivuta hisia za wapenda hip-hop nchini Tanzania baada ya kusema kwenye mahojiano hayo kuwa wasanii wa kike Tanzania wanaofanya hip-hop wakipewa nafasi watafanya vizuri kimataifa kuliko wasanii wa kiume.

"Na mimi naamini kutoka moyoni na naisema hii kauli hapa marapa wa kike Tanzania ni wakali kwenye level ambayo kama tunataka kupeleka rappers international take girls. Wana nafasi kubwa na ukali wao kuliko wanaume, straight up," alisema Frida.

Frida ni mojawapo kati ya wasanii wachache wa kike wanaofanya hip-hop nchini Tanzania na tangu aanze muziki, ameshatengeneza nyimbo nyingi zilizopata umaarufu kama ‘Bad’, ‘Anakudanganya’ pamoja na ‘Madam President’.

Leave your comment