Ommy Dimpoz Atangaza Mwezi Atakayoachia Albamu Yake Mpya

[Picha: Ommy Dimpoz Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Bongo Ommy Dimpoz hatimaye ametangaza kuwa atarejea kwenye tasnia ya muziki. Ommy Dimpoz amekuwa kimya kwa muda mrefu na mashabiki wake walikuwa wameanza kuonyesha wasiwasi.

Soma Pia: Ommy Dimpoz Akanusha Madai ya Uhasama Baina Yake na Alikiba

Baadhi ya watu walikuwa wamemuuliza iwapo amestaafu kutoka kwa tasnia ya burudani. Katika mahojiano na Simulizi Na Sauti, Ommy Dimpoz alifafanua kwamba hajastaafu kutoka kwenye muziki. Alieleza kwamba amekuwa akishughulikia albamu yake.

Kulingana na Ommy Dimpoz, albamu hiyo itakuwa tayari ifikapo mwezi wa tisa na kwa hivyo mashabiki wake wajiandae kumkaribisha tena.

Alipoulizwa kwanini alikaa kimya kwa muda mrefu, Ommy Dimpoz alidai kwamba anataka kujiandaa kikamilifu kabla ya kurudi kwenye muziki. Mwimbaji huyo alifunua zaidi kuwa anafanya kazi na wadau mbali mbali katika tasnia ya muziki kwenye albamu yake.

Soma Pia: Ommy Dimpoz Atia Kando Ugomvi wake na Diamond

Alisema pia kwamba ameunda studio yake ya kibinafsi ambapo anarekodi nyimbo.

"Yaani nataka nikwambie nakuja na album kali. Na the good thing miaka ya sasa hivi kuna writers, producers, unaweza kufanya kazi kisasa. Na nimekuwa nikikutana na hayo maswali, oh Ommy Kazi mpya vipi? lakini nimekuwa nikipata time nikirecord album yangu taratibu. Na nika ahidi kuna time kuwa album inakuja hivi karibuni. Lakini kulingana na mazingira ambayo yapo sasa hivi natarajia mwezi wa tisa," Ommy Dimpoz alisema.

Leave your comment