AT Awasihi Wazanzibari Kumuunga Mkono Harmonize

[Picha: AT Mfalme Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Tanzania AT amejitokeza kuwahimiza mashabiki wake kutoka Zanzibar kumuunga mkono Harmonize. Katika habari iliochapishwa kwenye ukurusa wake Instagram, AT alimthamini Harmonize kwa kusaidia kazi yake ya muziki na kumrudisha kwenye tasnia ya burudani.

Soma Pia: Harmonize Ajibu Madai ya Kununua Watazamaji YouTube Kwenye Wimbo wake ‘Sandakalawe’

AT ambaye ni mmoja wa wanamuziki wakongwe katika tasnia ya muziki wa Tanzania, alikuwa amekaa kimya kwa muda mrefu sana, kisha Harmonize alimkaribisha kwenye lebo yake ambapo aliachia kolabo aliyomshirikisha Anjella kutoka lebo hiyo.

Ushirikiano huo ulimrudisha AT na kumfanya kuwa mmoja wa wanamuziki wanaojadiliwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Katika ujumbe wake ambao alichapisha kwenye mtandao wa Instagram, AT alitoa shukrani pia kwa usimamizi wa lebo ya Konde Worldwide pamoja na vyombo vyote vya habari ambavyo vilichangia kufufua taaluma yake ya muziki.

Soma Pia: Anjella Amshirikisha AT "Si Saizi Yako’: Nyimbo Mpya Tanzania [Official Audio]

"Nimekuwa nikifanya kazi kwa Kuzingatia Ukubwa wako na Heshima ya Watu wetu wote Nichukue nafasi hii kukushukuru wewe @harmonize_tz na kila shabiki wako na Uwongozi Mzima Kwa kufanya Leo AT azungumzike atizamike Upya pamoja na kuwashukuru kwa Dhati Media's Zote," AT alisema.

Aidha, AT aliendelea kwa kuwasihi wafuasi wake kutoka Zanzibar wamuunge mkono Harmonize na kuelezea kuwa yeye ni mmoja wa wanamuziki wachapakazi katika tasnia ya burudani ya Kitanzania.

"Wazanzibar Naomba Niwaambie Tu Huyu Kijana Ni ndugu yetu anaroho ya kipekee Tokea nimekuwa nae karibu na Kuna Makubwa kwa Bara na Visiwani kwetu Get ready msirubuniwe Njooni nilipo Nasema CHECHEI kila Mmoja aitikie CHECHEI Tusonge mbele," aliongeza.

Leave your comment