Joeboy Kutumbuiza Katika Tamasha la Nandy Festival Arusha

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Bongo Nandy amethibitisha kuwa mwimbaji wa Nigeria Joeboy atatumbuiza kwenye Tamasha lijalo la Nandy Festival litakalofanyika jijini Arusha.

Katika taarifa ambayo alichapisha kwenye mitandao ya kijamii, Nandy alisema kuwa Arusha ilimteua Joeboy kuwaburudisha mashabiki mwishoni mwa wiki hii.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Wimbo Mpya ‘Nimekuzoea’ Toka EP ya ‘Taste’

Tamasha la Nandy litafanyika Jumamosi, tarehe kumi mwezi wa Julai kwenye uwanja wa Eden Garden.

"Arusha imemteuwa @joeboyofficial kutoka Nigeria kutoa burudani Nandy Festival katika viwanja vya Eden Garden tarehe 10/7/2021 watakaaatu," Nandy aliandika kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii.

Nandy na Joeboy ni wasanii wenye mahusiano mazuri. Hapo awali, walishirikiana na kutoa wimbo uliopewa jina la Number One.

Wimbo huo ambao ulitolewa miezi mitano iliyopita kwa sasa una watazamaji takriban milioni sita kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Babu Tale Amsifu Nandy Baada ya Tamasha Yake ‘Nandy Festival’ Kufanya Vyema

Toleo lijalo la Tamasha la Nandy linatarajiwa kuwa moja ya kubwa zaidi ikizingatiwa kwamba kuna wasanii wengi kutoka nje ya Tanzania ambao wataburudisha kwenye tamasha hilo.

Nandy hadi sasa ametoa orodha ya wanamuziki ambao wataburudisha mashabiki na inaonekana kwamba wakati huu aliamua kuvuka mipaka ya Tanzania. Baadhi ya wasanii watakaoburudisha kwenye Tamasha la Nandy ni pamoja na Masauti, Tanasha Donna, Linah, Rosa Ree, Mr. Blue na wengine wengi.

Nandy amesifiwa na wadau mbali mbali katika tasnia ya burudani kutokana na kufanikiwa kwa matamasha ya Nandy Festival.

Leave your comment