Shetta Azungumzia Madai ya Kuacha Muziki na Kuingia Katika Siasa

[Picha: Shetta Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Tanzania Shetta amekanusha taarifa kuwa ana mpango wa kuacha muziki na kuingia katika uongozi na siasa. Akizungumza wakati wa mahojiano ya hivi karibuni, Shetta alidai kwamba watu walikuwa wakitafsiri vibaya nia yake nzuri ya kuwasaidia watu.

Soma Pia: Watu 7 Mashuhuri Waliompongeza Diamond Licha ya Kukosa Tuzo la BET

Ripoti hizo ziliibuka muda mfupi baada ya mwanamuziki huyo kuzindua kampuni yake iliyopewa jina la ‘Sawa’ ambayo lengo lake kuu ni kusaidia kupunguza ubaguzi na ukatili dhidi ya wanawake.

Kulingana na Shetta, alipata wazo la kuwasaidia wanawake katika jamii muda mfupi baada ya kushirikiana na mwanamuziki wa Afrika Kusini Emtee kwenye wimbo wake uitwao "Sikupingi Tena".

Soma Pia: Ommy Dimpoz Akanusha Madai ya Uhasama Baina Yake na Alikiba

Kujitolea kwa Shetta kusaidia wanawake katika jamii na wale walio na hali duni kumezua madai kwamba huenda alikuwa akifanya kampeni ya nafasi ya uongozi.

Mwanamuziki huyo, hata hivyo, amedai kuwa hana mpango wa kuacha muziki. Aliongeza kuwa yuko tayari pia kuwatumikia Watanzania katika nafasi ya uongozi ikiwa nafasi itapatikana.

"Sijafikiria huko, nimefikiria kuwafikia watu, kuwasaidia watu. Na ikifika time ambayo unaona unaweza kuwasaidia watu wengi kimamlaka why not. Lakini dhima na lengo ni kuwasaidia watu na sijafikiria ata hilo," Shetta alisema.

Aliongeza kuwa kila wakati amekuwa akiwasaidia watu kwa muda mrefu sana bila kutarajia malipo yoyote.

 Ripoti hizo zinaibuka muda mfupi baada ya kuteuliwa kwa mwanamuziki wa Hip-hop Nikki Wa Pili kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe. Nikki alikuwa mshiriki wa kikundi cha Weusi kabla ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu.

Leave your comment