Jokate Mwegelo Ampongeza Nikki wa Pili Kwa Kuteuliwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe

[Picha: Weusi Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Jokate Mwegelo ambaye alikuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe kabla ya kuhamishiwa Temeke, Dar es Salaam amejitokeza kumpa mkuu mpya wa Kisarawe Nikki Wa Pili ushauri juu ya uongozi.

Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni, Jokate Mwegelo alimpongeza Nikki wa Pili ambaye ni mwana chama wa kundi cha Hip Hop cha Weusi, kwa nafasi hiyo mpya. Alifunua kwamba amekuwa akishirikiana na Nikki na alikuwa na ujasiri kwamba alikuwa mtu sahihi kwa kazi hiyo.

Soma Pia: Jokate Mwegelo Azungumzia Uteuzi wa Wasanii Katika Uongozi Nchini Tanzania

Alisema kuwa alivutiwa na ajenda ya Nikki ya kukuza taasisi ya kisayansi katika wilaya ya Kisarwae.

"Nimefurahi yeye mwenyewe Nikki ameelezea kipaumbele chake ni masuala ya ujuzi, masuala ya sayansi na teknolojia, kwa sababu kwa kweli dunia sasa hivi ilivyo bila ujuzi, bila sayansi na teknolojia ni kujidanganya, kwa sababu ndio dunia iliko, ndio dunia inakoelekea. Kwa hivyo mimi nimefurahi Nikki hivyo ndivyo vipaumbele vyake," Jokate Mwegelo alisema.

Soma pia: Nikki wa Pili Kubaki na Kikundi cha Weusi Licha ya Kuapishwa Mkuu wa Wilaya

Wiki iliyopita, Rais Samia Suluhu alimteua Nikki wa kuwa mkuu wa Kisarawe siku chache zilizopita. Uteuzi huo ulikaribishwa na wadau wengi katika tasnia ya muziki wa Tanzania ambao pia walimshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuwatambua wanamuziki na kuwatunuku nyadhifa hizo za uongozi.

Leave your comment

Top stories

More News