Gigy Money Aomba Kuondolewa Adhabu na BASATA

[Picha: Muziki Mpya]

Mwandishi: Brian Sikulu

Mwanamuziki wa Tanzania Gigy Money ameibua hisia tofauti miongoni mwa mashabiki wake baada ya kulalamikia kuongezeka kwa adhabu dhidi yake.

Gigy Money alipgiwa marufuku ya miezi 6 kutotumbuiza kwenye hafla yoyote ndani ya Tanzania na BASATA baada ya kupanda jukwaani akiwa amevaa mavazi ya kutatanisha.

Soma Pia: Alikiba, Abdukiba, K2ga na Tommy Flavour ‘Ndombolo’: Nyimbo Mpya Tanzania

Adhabu ya Gigy Money ilitarajiwa kumalizika tarehe 5 mwezi wa Mei.

Gigy Money, katika taarifa kwa mtandao wa kijamii ambayo baadaye alifuta, alidai kuwa juhudi za kuwasiliana na maafisa kutoka BASATA hazijafaulu.

Aliendelea kuuliza ni kwanini adhabu yake inaonekana imeongezwa na kwanini BASATA haijawasiliana naye licha ya tarehe ya mwisho ya marufuku yake.

Soma Pia: Lava Lava ft Mbosso 'Basi Tu': Nyimbo Mpya Tanzania [Video]

Gigy Money alisema kwamba alikuwa amekiri makosa yake na amebadilisha tabia yake. Hata hivyo, alihoji ikiwa anapuuzwa kwa sababu hana pesa.

"Simuh azishikwi, kwani mm sio mtanzania kwanini haki yangu inakua ngumu kuipata kisa sina pesa yakuwapa au???? Na mnajua mm napitia rain mwanangu asomi kasimamishwa shule, mdada kaondoka sijamlipa miezi4 pango la nyumba sine ninekuja kuishi kwa marafiki Na mwanangu je kuna anaejua naogopa ata kukopa kwani hii vita kama mnanichukia mimi kama kosa langu nilikubali Na nikajirekebisha Na miezi 6 mmenifungia sasa kwanini hamniiti tena kama mnavyoniitaga mbona tars imepita mpo kimya au kisa sina iyo milioni moja," Gigy Money alisema.

Gigy ameongeza kuwa anamkumbuka marehemu Rais John Magufuli ambaye alijali ustawi wa wanamuziki.

Leave your comment