Barnaba Afunguka Kuandikiwa Nyimbo na Wasanii Wengine

[Picha: Barnaba Classic Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Tanzania Barnaba Classic amefunguka kuhusu taarifa zinazoashiria kuwa nyimbo zake huandikwa na wanamuziki wengine.

Akizungumza na wanahabari hivi karibuni, Barnaba alikiri kwamba kweli anashirikiana na wanamuziki wengine katika kuandika nyimbo zake. Aliendelea kwa kutoa mfano wa wimbo wake wa hivi karibuni uliopewa jina la 'Cheketua' ambao aliutoa kwa kushirikiana na Alikiba.

Read Also: Barnaba Classic Aahidi Kumpigia Diamond Kura Kwenye Tuzo za BET

Alifunua kuwa msanii Mulla alichangia pakubwa sana katika kuandika wimbo huo.

"Kwa mfano kama Cheketua, asilimia 35 alioshiriki kuuandika ni msanii wangu mdogo hajatoka bado anaitwa Mulla. Yule Mulla ndio ame participate kuandika Cheketua," Barnaba alisema katika mahojiano hayo.

Kulingana na Barnaba, ushiriki wa wasanii wengi haswa kutoka kizazi cha sasa katika kuandika wimbo ni mzuri. Barnaba alibaini kuwa amekuwa kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu sana na kulikuwa na mambo katika kizazi cha sasa ambacho hajui.

Read Also: Barnaba Afichua Changamoto Kuu Katika Tasnia ya Burudani Tanzania

Alisema kuwa wanamuziki wachanga watasaidia kujaza nafasi hiyo tupu kwa kufanya nyimbo zake ziweze kurejelewa na hadhi ya sasa ya burudani. Barnaba aliwataka wanamuziki wengine kuwa tayari kila wakati kusaidiana katika kuandika nyimbo.

Kwa sasa, Barnaba anatamba na wimbo wake mpya ‘Cheketua’ aliyomshirikisha Alikiba. Ngoma hiyo imepokelewa vizuri na inawatazamaji zaidi ya milioni moja nukta saba kwenye YouTube ndani ya wiki moja.

Leave your comment