Barnaba Classic Aahidi Kumpigia Diamond Kura Kwenye Tuzo za BET

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki tajika kutoka Tanzania Barnaba Classic ametangaza kuwa atampigia kura Diamond Platnumz kwenye Tuzo za BET.

Akizungumza wakati wa mahojiano ya hivi karibuni, mwanamuziki huyo alisema kuwa anajivunia mafanikio ya Diamond kama msanii. Alidokeza kuwa watu hawapaswi kumwona Diamond kama mwanamuziki mmoja, bali wanapaswa kumwona kama mwakilishi wa Tanzania.

Soma Pia: Barnaba Afichua Changamoto Kuu Katika Tasnia ya Burudani Tanzania

Barnaba alieleza kuwa sababu ya kumpigia kura Diamond ni kwamba anataka Tanzania iwekwe kwenye ramani ya kimataifa. Mwimbaji huyo wa 'Cheketua' alisisitiza kuwa ushindi kwa Diamond ni ushindi kwa Watanzania wote.

Alitoa wito kwa wadau mbali mbali katika tasnia ya burudani kuungana na kuhakikisha kuwa Diamond anashinda tuzo hiyo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu, Diamond, Alikiba na Wasanii Wengine Wanoatarajiwa Kuachia Ngoma Mpya

"Mimi kumwona Diamond leo kwenye BET, sisemi Diamond ananominate BET, nasema Tanzania ina nominate BET. Kwa hivyo niko very proud na niko na furaha na nitaipiga kura yangu kwa mtu kama Diamond kwa sababu, hashindi Diamond, inashinda Tanzania," Barnaba Classic alieleza.

Ufafanuzi wa Barnaba unakuja wakati uteuzi wa Diamond kwenye BET umepata utata kati ya Watanzania. Sehemu ya watanzania wameanzisha kampeni kwenye mitandao ya kijamii kwa kujaribu kumfanya Diamond aondolewe kwenye tuzo hiyo ya kifahari.

Walidai kwamba anapaswa kutupwa nje ya tuzo hiyo kwa kuunga mkono serikali ya Rais wa zamani wa Tanzania John Magufuli. Diamond Platnumz hadi sasa hajazungumzia suala hilo.

Leave your comment