Nyimbo Mpya: Killy Aachia ‘Roho’, Wimbo Wake wa Kwanza Tangu Kujiunga na Konde Worldwide

[Picha: Killy Instagram]

Mwandishi: Omondi Otieno

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Killy kutoka lebo ya Konde Music Worldwide ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Roho’.

Kwenye wimbo huu, Killy anamkashifu mpenzi wake kwa kumuacha bila kumueleza ni kwanini ameondoka.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Zuchu, Rayvanny, Mbosso na Lava Lava Mwezi Mei 2021 [Video]

Analia kuwa baada ya mpenzi wake kuondoka, maisha yake yamebadilika sana na bado ‘Roho’ yake inauma.

Wimbo huu una ushairi wa hali ya juu na mistari yake ina ujumbe inayoleta hisia za huzuni.

“Kipi nimetenda kibaya au kukupenda nlifanya vibaya dah. Eti na nguo sizioni umefungasha virago vyote umefunga funga. Umeniacha kwa ubaya ila sina budi kukubali haya aah… Umeondoka bila kusema sababu iliyokufanya uende. Ungeandika hata barua ningeisoma nitake ama nisipende. Hata kama umenichoka ya nyuma ungevuta taswira,” aliimba Killy.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Kali Zilizoachiwa na Wasanii wa Konde Gang Mei 2021[Video]

Mdundo wa ngoma huu uliandaliwa na Terriyo kutoka Imaging Sound. ‘Roho’ imepokelewa vizuri na inawatazamaji zaidi ya laki moja masaa kadhaa baada ya kuachiwa.

Kand ya video hii bado haijaachiwa. Inakisiwa kuwa kanda hiyo itatoka hivi karibuni.

‘Roho’ ni ngoma ya kwanza kuachiwa na msanii Killy tangu ajiunge na lebo ya Konde music Worldwide baaada ya kutoka lebo ya Kings Music chini ya uongozi wake Alikiba.

Wiki kadhaa iliyopita, Mkurugenzi mkuu wa Kinde Music Worldwide Harmonize alitangaza kuwa Killy, Cheed, Anjella na Ibraah wamekamilisha alabamu zangu na watakuwa wakiziachia baadaye mwakani.

https://www.youtube.com/watch?v=ZA-xQAvmsTw

Leave your comment