Alikiba Athibitisha Uwepo Wake Kwenye Tamasha la Nandy Festival

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota nchini Tanzania Alikiba amejitokeza kumuunga mkono msanii Nandy kabla ya tamasha lake la Nandy Festival 2021 litakalofanyika Jumamosi huko Kigoma.

Kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, Alikiba aaliwaomba watanzania kujitokeza kumuunga mkono Nandy.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Kali Zilizoachiwa na Wasanii wa Konde Gang Mei 2021[Video]

Kulingana na Alikiba, tasnia ya muziki wa Tanzania ina uhaba wa waimbaji wa kike na kwa hivyo wale wachache waliopo wanapaswa kuungwa mkono.

Alielezea kuwa wanamuziki wa kike wanapaswa kuwezeshwa ili kufanikiwa zaidi kujenga mazingira mazuri kwa waimbaji wengine wachanga wa kike.

Alikiba alizidi kumsifia Nandy kwa kuwa msanii anayejituma na kufanya kazi kwa bidii. Nyota huyo aliendelea kusema kuwa anapenda kazi ya Nandy na ndio sababu atatoka kutumbuiza kwenye hafla yake.

Soma Pia: Diamond Platnumz Ateuliwa kwa Tuzo za BET 2021

"Sanaa yetu ina upungufu wa wasanii wa kike, inabidi waliopo wapewe nguvu ill waweze kufanikiwa zaidi. @officialnandy ni msanii anayejituma na mwenye jitihada. Napenda anachofanya na ndio maana Jumamosi ijayo nitaenda nyumbani Kigoma kumpa support katika #NandyFestival," Alikiba alisema.

Nandy kwa kujibu taarifa hiyo alimthamini Alikiba huku akimtaja kama kaka yake mkubwa katika tasnia ya muziki.

Alisema kuwa alinyenyekezwa na ishara hiyo pia aliwahimiza mashabiki wake wajitokeze kwa wingi kwenye hafla hiyo.

Nandy ni miongoni mwa wanamuziki nguli wa kike nchini Tanzania. Mpinzani wake mkuu ni Zuchu kutoka WCB ambaye pia anafurahiya umaarufu mwingi.

Leave your comment