Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Kali Zilizoachiwa na Wasanii wa Konde Gang Mei 2021[Video]

[Picha: InstaBongo]

Mwandishi: Omondi Otieno

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wasanii wa Bongo Fleva wanaendelea kuonyesha umahiri wao eneo la Afrika Mashariki kwa kuachia ngoma mpya zinazotamba.

Mwezi huu ulioisha wa Mei, wasanii kadhaa wameachia nyimbo mpya. Katika nakala hii, tunaangazia nyimbo zilizoachiwa na wasanii wa Konde Music Worldwide zinazotambaa Tanzania:

Soma Pia: Rayvanny Atajwa Msanii wa Pili Bongo Mwenye Mauzo Makubwa ya Muziki

Attitude - Harmonize ft Awilo Longomba and H Baba

‘Attitude’ ni mojawapo ya nyimbo bora zilizoachiwa Bongo mwaka huu. Ndani ya mwezi mmoja, wimbo ‘Attitude’ wa Harmonize umefikisha watazamaji zaidi ya milioni kumi na moja kwenye YouTube. Katika wimbo huu, Harmonize aliwashirikisha wasanii Awilo Longomba na H-baba.

https://www.youtube.com/watch?v=bElhxzQweYQ

Nobody - Anjella

Hii ni kazi yake Anjella kutoka Konde Gang iliyopokelewa kwa ukubwa sana. ‘Nobody’ ni wimbo wa mapenzi na kufikia sasa una watazamaji zaidi ya milioni tatu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=-NCqC_BoUXc

Do Lemi Go - MC Kinata ft Ibraah

Huu ni wimbo wa Singeli wake MC Kinata ambao alimshikisha Ibrah kutoka Konde Music Worldwide. Kwenye mistari yao Kinata, anaimba kuhusu upendo huku Ibraah akitupa michambo. Kufikia sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya laki tatu kwenye YouTube.

Soma Pia: Wasifu wa Rose Muhando, Nyimbo Zake Bora, Albamu Zake, Tuzo Alizoshinda,Changamoto Alizopitia na Thamani Yake

https://www.youtube.com/watch?v=VubqA0ej12w

Bado – Country Wizzy ft Seyi Shay

Hii no mojawapo ya nyimbo kutoka kwenye ‘Father’ EP yake Country Wizzy. Video hii iliachiwa wiki moja iliopita na ina zaidi ya watazamaji laki tatu.

https://www.youtube.com/watch?v=KtHUEzcl78Y

Mapenzi – Ibraah

Kama jina inavyoashiria, wimbo huu ni wa wapendanao. Ibraah ametumia ushairi wa hali ya juu kuzungumzia mapenzi. Video hii imepokelewa vizuri na inawatazamaji zaidi ya laki nane kwenye YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=q_0A3pvSehs

Leave your comment