Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TMK Warejea! Juma Nature Amshirikisha Chege Kwenye Wimbo mpya ‘Kucha’ [Video]
26 May 2021

[Picha: Juma Nature Instagram]
Mwandishi: Branice Nafula
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Nguli wa mziki wa Hip-hop Juma Nature ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Kucha’ akimshirikisha aliyekuwa katika kundi lake TMK Wanume Halisi Chege Chigunda.
‘Kucha’ ni wimbo ambao wawili hawa wanamsifia binti ambaye wamependezwa naye. Ukiskiliza na kuitazama kanda ya wimbo huu, ufundi na ushairi wa wasanii hawa unadhihirika.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Zilizoachiwa Bongo Wikendi Iliyopita [Video]
Juma Nature anaanza kwa kusifia uno la mrembo mmoja ambaye kulingana naye ni binti halisi kwani ni dada amelelewa kipwani. Vile vile anasafia jinsi alivyo na maumbile ya kuvutia.
“Hataki hataki watoto wadogo watampa nini huyo?? Ni pin kali huyo!! mkamate huyo!!” aliimba Nature.
Pia kupitia sweta alilovaa Nature kwenye kanda hii ametangaza kuwa kundi la wanamziki wa hip-hop TMK wamerejea.
Soma Pia: Wasifu wa Maua Sama, Nyimbo zake Bora, Mahusiano na Thamani Yake
Sweta hiyo alisoma ‘TMK is Back’. Chege kwa upande wake aliingia na mistari yake ya kifundi alipoendelea kumsifia binti huyo mrembo.
Kanda ya wimbo huu ilifanywa kwa ustadi mkubwa na mwelekezaji Joma wa Tanzania na ilitengezwa mjini Dar es Salaam.
Wakati mashabaki wanaendelea kuupokea wimbo huu kwa kishindo, ni muhimu kukumbuka kuwa Juma Nature ni msanii mojawapo aliyepeperusha mziki wa Tanzania kwa ustadi mkubwa miaka ya nyuma.
Anaporejea kwenye ulingo wa mziki heshima na hadhi yake itabaki kusifiwa. Kwa sasa wimbo ‘Kucha’ una watazamaji zaidi ya laki moja.
v=xLJHc4DDfts&ab_channel=ChegeChigundaChegeChigundaOfficialArtistChannel
Weekly Top 10 songs

KAPEKE LONDON2:23
BIkola2:58
In My Bed2:50
Buwooma2:44
Ex Nkubilako ft DonMusa2:55
Baddie remix feat Shannnon, aaronix, Tojo3:14
CHAMPION GAL3:00
Paver2:55
Nitampeleka kwa Mama (ft. Xouh)3:44
Joy Is Coming3:08
Top stories
- NEW SONG ALERT
16 May
- Generation
16 May
- Boom Shakatah means
17 May
- Date of birth
15 May


Leave your comment