Wasifu wa DJ Ally B, Shows na Tamasha Zake Kubwa

[Picha: DJ Ally B]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

DJ Ally B ni nani na ana miaka mingapi?

Jina la usani: DJ Ally B

Jina halisi: Ally Seleman Simba

Tarehe ya Kuzaliwa:16-03-1986

Mix tapes zake ni za muziki gani: Naija

Soma Pia: Wasifu wa DJ Massu, Kazi na Show Zake Kubwa

DJ Ally B alianzaje kazi yake ya kuwa DJ na lini?

DJ Ally B ni mzoefu wa kucheza santuri na ameachia kazi mingi kufikia sasa. Kitaalam, amefanya kazi ya kuwa DJ karibu kufika miongo miwili kwenye jukwa tofauti kama vile tamasha za muziki na hata kwenye sherehe mbalimbali  nchini Tanzania. Vilabu alizofanya nazo kazi ni kama vile Laliga mjini Moshi, Tripple A Arusha, Rock Bottoms ya Mwanza, Elements, High Spirite na Havoc and  Buckets jijini Dares Salaam. 

Soma Pia: Wasifu wa DJ Summer TZ, Show Zake Kubwa na Tuzo Alizoshinda

Ally B amefanya kazi na wasanii gani?

Ally B anajivunia kama mwanasanturi wa kimataifa  na ameshirikishwa kwa majukwaa mbali mbali. Katika kazi yake, amepata fursa ya kujumuishwa na kufanya kazi na wasanii wengine maarufu kama vile DJ Maphorisa wa Afrika Kusini, Sauti Sol wa Kenya, Patoranking na Maleek Berry kutoka Nigeria.

Soma Pia: Wasifu wa DJ Feruuh, Nyimbo Zake Bora na Show Zake Kubwa

Ni vituo gani za Habari Ambazo DJ Ally B amefanya kazi nazo?

Ally B amebarikiwa kufanya kazi na stesheni kadhaa za redio kama vile; Triple A Fm, Kiss Fm, Passion  Fm, Times Fm, TBC Fm na E FM. Vile vile alifanya kazi kwenye vituo vya runinga kwa vipindi vya DTV vinavyojulikana kama Extreme live.

Show zake kubwa ni kama gani?

DJ Ally B amecheza kwa tamasha tofauti za muziki zikiwemo Life of the Beach,Mziki Mnene, Wasafi Festival, Budx Party na Castle Lite Unlocks ya Afrika Kusini.

Ally B hufanya nini wakati wake wa Ziada?

Katika kukuza sanaa DJ Ally B hutumia pia wakati wake kujifunza vitu vipya. Pia anamiliki chuo cha DJ kinachojulikana kama Simba Scratch Academy  anayotumia kuwafundisha wale wanaopenda na kutamani kuwa ma DJ.  

Leave your comment