Wasifu wa DJ Summer TZ, Show Zake Kubwa na Tuzo Alizoshinda

[Picha: DJ Summer TZ]

Mwandishi: Omondi Otieno

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

DJ Summer TZ ni nani na ana miaka mingapi?

Jina la usani: DJ Summer TZ

Jina halisi: Immanuel John 

Mix tapes zake ni za muziki gani: Bongo 

DJ Summer alianzaje kazi yake ya kuwa DJ na lini?

DJ Summer alianza rasmi kazi yake ya  kuDJ mwaka wa 2005 katika mji wa Arusha, Tanzania. Hivyo, anajivunia kuwa na tajriba ya zaidi ya miaka kumi na mitano katika kazi hii. DJ Summer anatambulika kwa kucheza kwenye vilabu tofauti tofauti Tanzania. Kwa sasa, ni mmoja wa madj tajika nchini Tanzania na eneo la Afrika Mashariki.

Kando na kucheza kwenye vilabu, DJ Summer TZ pia amebarikiwa kufanya kazi na stesheni kadhaa za redio. Kwenye miaka kumi na tano aliokuwa kwenye kazi hii, DJ Summer amebahatika kufanya kazi na MJ Radio (Arusha), Kiss FM (Mwanza) na East Africa TV and East Africa Radio 2012 ambapo ndipo anafanya kazi sasa.

Soma Pia: Wasifu wa DJ Feruuh, Nyimbo Zake Bora na Show Zake Kubwa

Tuzo Alizoshinda

STR8 Music DJ Competition 2010-2011 

Show zake kubwa ni kama gani?

Planet Bongo

Yeyote anayetaka kumskiza DJ Summer anaweza mpata hewani siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kwenye show ya Planet Bongo masaa ya saa saba hadi saa kumi mchana. Show hii ni ya muziki wa Bongo pekee.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Zinazovuma Bongo Wiki Hii [Video]

The Cruise

Pia unaweza mskiza DJ Summer kwenye show ya The Cruise siku ya Jumatatu hadi Ahlamsi majira ya saa tatu hadi saa sita mchana.

Top Playlist 

Show hii iko siku ya Jumapili kuanzika saa nne hadi saa nane mchana. Kwenye show hii, DJ Summer anacheza mchanganyiko wa muziki mpya pekee.

Friday Night Live

Show hii iko siku ya Ijumaa kuanzia saa saa tatu hadi saa tano usiku. Show hii hupeperushwa moja moja kwenye stesheni ya TV.

Leave your comment

Top stories

More News