Innoss’B Atua Bongo Kuchapa Collabo na Rayvanny na Diamond

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msani tajika kutoka Bongo Rayvanny amemkaribisha msanii wa Congo Innoss’B kwa ajili ya kufanya kazi ya pamoja.

Rayvanny ametaja kuwa Innoss'B ni miongoni mwa wasanii nyota watakaoshirikishwa kwenye album ijayo ya nyota wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz.

Fungu la Leo Zaburi 118:14

“Plani ni kufanya kazi after kazi , kama unamuona hapa Innoss, tuko na Kelebe lakini ni more than Kelebe…” alisema Rayvanny

Innoss'B ametua jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumalizia baadhi ya kazi alizoshirikishwa na Rayvanny ikiwemo kufanya video ya wimbo wao.

Soma Pia: Konde Music Worldwide Kuachia Albamu Nne Mwaka wa 2021

Rayvanny alimshirikisha muimbaji huyo wa ‘Yope’ kwenye album yake ya kwanza, 'Sound From Africa' iliyotoka rasmi February 1, 2021, katika wimbo wao ‘Kelebe’.

Vile vile, Innoss’B ameahidi kuwa kuna kazi zingine zaja ndani ya Wasafi na wasanii wengine wa lebo tofauti.

“Just like Rayvanny amesema for me Tanzania is home and just like we linked up with Diamond and made a big hit, expect more from me as long as vile amesema our spirits zetu zinakutana tegea tunaleta vitu vizuri I mean ‘Kelebe’ is a big tune expect kazi nzuri…” alisema Innoss’B.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lava Lava Aachia Video Mpya ‘Komesha’

Innoss’B anasifika Tanzania baada ya colabo yake na Diamond kwenye wimbo wa ‘Yope’ remix.

‘Yope’ Remix kwa sasa ndio wimbo wenye watazamaji wengi kanda la Afrika Mashariki.

Leave your comment