New School Vs Oldskul Bongo: Tofauti 3 Kuu Kati ya Bongo Fleva ya Kisasa na Ile ya Awali

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Muziki wa Bongo Flava umekua kwa kasi nchini Tanzania na hata katika hadhira ya kimataifa. Muziki huu umepata fursa ya kutamba katika mataifa mengi ulimwenguni ila kwa sasa kuna tofauti kubwa kati ya mziki wa Bongo wa mwongo moja iliyopita na bongo flava ya sasa.

Pata Ubashiri wa Mechi Kati ya Real Madrid na Chelsea 

Katika nakala hii, tunaangazia tofauti kuu ya bongo fleva ya kisasa na ile ya kaizazi kilichopita:  

Fungu la Leo Zaburi 118:14

Muziki wa Haraka

Bongo Fleva ya kisasa ina midundo ya haraka, hivyo kuifanya kuwa muziki unaopendwa na wengi hasa wasakata densi. Hii imefanya muziki huu kukubalika eneo la Afrika Mashariki na barani Afrika kwa jumla. Muziki huu wa haraka ndio unaovuma sasa, hivyo iliwabidi wanamuziki wa Bongo kugeuza mitindo yao ilikuambatana na muziki unaotamba wakati huu. Awali, muziki huu ulikua wa kuelezea tu maudhiui yanayogusia masuala ya kijamii kama vile mapenzi, ugonjwa kama vile HIV, ufisadi miongoni mwa mengineyo.

Soma Pia: Muziki wa Singeli Tanzania: Kwa Nini Singeli Haitambi Kama Bongo Fleva?

Lugha Tumika

Muziki wa Bongo fleva wa Kizazi kilichopita kilitumia sana lughya ya Kiswahili. Ushairi ulitumika kuimarisha mistari ya nyimbo zilizoachiwa wakati huo. Lugha ya Kiswahili ilitumika sana wakati huo wa kuwa muziki wa Bongo bado haukuwa umetamba barani Afrika, hivyo wasikilizaji wengi walikuwa kutoka nchi ya Tanzania na Kenya.

Soma Pia: Wasifu wa Vanessa Mdee, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Kwingineko, Bongo Fleva ya kizazi kipya ina mchanganyiko wa lugha. Wasanii wengi wa Bongo wameanza kupitia lughya ya Kingereza na ndimi zingine ili kuwafikia wasikilizajji wengi duniani kote. Kutumia lugha nyingine pia inafanya nyimbo zao kupata umaarafu na kuongeza nafasi ya wasanii hao kutuzwa kwenya tuzo kubwa kubwa duniani kama vile Grammys, BET na kadhalika.

Mapato Kutokana na Muziki

Awali, muziki wa bongo ulizingatia uandishi wa ushahiri dhabiti bila ya kuwazia iwapo mziki utaleta mauzo au la. Lakini miaka zinapoendelea kubadilika, wasanii wanalazimika kufanya mziki kulingana na nyakati zake na mapato watakopata kutokana na ngoma zao. Kwa sasa, tunaona muziki ambao ni wa kusambaa kwa muda mfupi, kupata mauzo yake na kutokomea. Kisha baadaea wanaachia nyingine ili kuwa kwenye orodha ya ngoma zinazovuma (trends).  

Leave your comment