Wasifu wa Harmonize, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

 Harmonize ana umri gani na ametoka wapi?

Jina la usani: Harmonize

Jina halisi: Rajab Abdul Kahali

Tarehe ya kuzaliwa: 3 Oktoba 1991 (miaka 30)

Aina ya muziki: Bongo Flava, Afro pop

Thamani: Harmonize anakisiwa kuwa na thamani ya dola milioni mbili.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Kali Kutoka Konde Music Worldwide Mwaka 2021

Harmonize ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo aliyezaliwa kwa Bwana na Bi Kahali mnamo mwaka wa 1991. Baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari katika Shule ya Mkundi mnamo 2009, Harmonize alihamia Dar es Salaam ambapo alianza kuuza bidhaa katika barabara za Soko la Kariakoo.

Harmonize alianza muziki lini?

Harmonize alianza kazi yake ya muziki mnamo 2011. Muziki wake haukupata mvuto sana. Baada ya kutafuta kwa muda, Harmonize alikutana na Diamond Platnumz mwaka wa 2015, akamskizisha Diamond kazi zake na akakubali kugharamikia kazi yake ya kwanza.

Baadae, Harmonize alienda Afrika Kusini mwaka huo na akaachia wimbo wake wa kwanza kabisa 'Ayiola' ambayo ilipata kucheza kote Afrika masahiriki. Kufikia mwaka wa 2016, alikua msanii wa kwanza kusajiliwa chini ya Wasafi Records ya Diamond. Alirudi Tanzania na kushirikiana na Diamond Platnumz kwenye ‘Bado’. Wimbo huu ulimpa Harmonize mwanga aliohitaji katika sana. Aliachia baadhi ya vibao bora chini ya lebo ya WCB kama vile; 'Matatizo' na 'Niambie'. Mwisho wa 2019, Harmonize aliondoka WCB kuanzisha studio yake ya Konde Music Worldwide.

Soma Pia:Tembo Vs Chui: Harmonize, Rayvanny Waachia Nyimbo Mpya ‘Vibaya’ na ‘Nyamaza’

Kwanini Harmonize Aliondoka Wasafi?

Ripoti zinaonyesha kwamba aliondoka Wasafi kutokana na kutokuelewana na uongozi wake wa awali; pia alitaka kujitegemea mwenyewe.

Harmonize alianzisha lebo ya Konde Music Worldwide lini?

Konde Music Worldwide ilianzishwa mnamo Septemba 2019, na kwa sasa ni mojawapo ya lebo tajika nchini Tanzania. Kwa sasa, Harmonize anajivunia kusajili wanamuziki wanaokua kwa kasi wakiwemo Ibraah, Killy, Cheed, Country Wizzy Anjella na Skales kutoka Nigeria. Vile vile, Harmonize anaendelea kuwa mmoja wa mastaa wa muziki wenye ushawishi mkubwa na wanaotafutwa sana.

Ni nyimbo zipi ambazo ni ushirikiano bora wa kimataifa za Harmonize?

Harmonize ameshirikiana na wasanii kadhaa wa kimataifa na walio bora ulimwenguni. Baadhi ya ushirikiano zake kubwa ni pamoja na; Burna Boy kwenye 'Kainama Remix', Skales na Falz kwenye Remix ya Oliver Twist, Khaligraph Jones, Spice Diana, kati ya wengine wengi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Kali Zinazovuma Bongo Wiki Hii [Video]

Albamu na EP Zake

  • Afro Bongo 2019
  • Afro East Album 2020
  • Bedroom EP 2020

Harmonize ana Tuzo Ngapi?

  • 2016 - WatsUp TV Africa Music Video Awards kwa Video Bora ya Mgeni wa Kiafrika
  • African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) kama Msanii mpya
  • African Entertainment Awards (AEAUSA) kama Msanii mpya bora zaidi

Harmonize anachumbiana na nani?

Awali, Harmonize alikuwa akichumbiana na mfanyi biashara na mwigizaji wa Kitanzania Jacqueline Wolper kabla ya kuanza kugombana kwa madai ya udanganyifu.

Baadaye, alichumbiana na mwanamitindo wa Mexico Sarah Michelotti lakini wakaachana. Kisha akaanza uhusiano na mwigizaji na mwanabiashara Bi. Fridah Kajala lakini uhusiano wao haukumaliza miezi mitatu kabla ya wao kuachana kwa tuhuma za kutaka kujihusha na binti wa Frida Kajala, Paula.

Kwa sasa inasemekana hayuko kwenye uhusiano ila ana mtoto mmoja aliyemtambulisha kama Zuu Konde.

Leave your comment