Nyimbo Mpya: Rose Muhando Aachia Video Mpya Kwa Jina ‘Simba’

[Picha: Rose Muhando Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii nguli wa injili kutoka Tanzania Rose Muhando ameachia kanda ya wimbo wake mpya kwa jina “Simba”.

Katika hali ya kujirudisha katika mziki ramsi Rose muhando aliachia albamu yake ya nane kwa jina “Miamba Imepasuka” yenye nyimbo kumi.

Soma Pia: Nyimbo za Injili za Kiswahili Kwenye Mdundo (Pakua bila Malipo)

‘Simba’ ni moja ya nyimbo kwenye albamu hiyo ambapo anasifia ukubwa wa mwenyezi Mungu.

Rose Muhando anawaitwa binadamu waje waone namna Mungu amemrejesha kwenye kazi yake ya kuimba na kumsifu.

“Mwambieni yule mbweha, nimerudi kutoka njangwani, Nimesimama tena kwenye zamu yangu, Wapeni habari wale umbwa,Hii si bahati mbaya, mbingu zimeniamini, Mungu amenidhibitisha…” aliimba Rose Muhando.

Soma Pia: Wasifu wa Diamond Platnumz, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Thamani na Mahusiano Yake

Kanda ya wimbo huu imetengezwa kwa ufundi mkubwa kuanzia kwa mandhari, mavazi na hata usakataji.

Rose Muhando anasisitiza kuwa yeye anajeuri ya kumcha Mungu na ndio fahari yake kubwa.

Rose Muhando anatukumbusha kumcha Mungu na kuamini kuwa sisi ni “Simba” katika maisha yetu. Mdundo wa wimbo ulifanyiwa utayarishaji na Producer Amos Mungwana na video ikaelekezwa na Ein -xer Maximum Vision wa EcK Production.

Kufikia sasa wimbo huu unaendelea kupata umaarufu kwenye mtandao wa YouTube na una watazamaji zaidi ya elfu ishirini na tano.

https://www.youtube.com/watch?v=I9KS9jNhEo8

Leave your comment