Wasifu wa Diamond Platnumz, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Thamani na Mahusiano Yake

[Picha: Diamond Platnumz Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Diamond Platnumz ana umri gani na ametoka wapi?

Jina la kisanii: Diamond Platnumz

Jina halisi: Naseeb Juma Abdul

Tarehe ya kuzaliwa: 2 Oktoba 1989 (umri wa miaka 30)

Aina ya muziki : Bongo Fleva, Afro pop, Afro beat

Thamani halisi: Takriban Dola za Kimarekani milioni 7

Diamond Platnumz alizaliwa Tandale, Dar es Salaam. Alisoma shule ya msingi ya Tandale Magharibi.

Diamond alianzaje kazi yake ya muziki na lini?

Diamond Platnumz alianza kuonyesha kupenda muziki akiwa katika darasa la 5. Mama yake Bi Sandra Dangote alipoona hili aliamua kumnunulia albamu kadhaa ili azisikilize. Hivyo, Diamond alitumia nyimbo hizo kuiga wasanii wengine na kuimbia wanafunzi wenzake shuleni. Baada ya shule, familia haikufikiria muziki ulikuwa biashara inayofaa kwa Diamond lakini mama yake aliendelea kumpa motisha ajiskume zaidi.

Kwa muda, Bi Dangote alimpeleka kwenye maonyesho ya talanta ili kukuza talanta yake wakati huo. Hatimaye Diamond aliachia wimbo wa kwanza ambao ulimweka kwenye ramani ya muziki, ‘Mbagala’ mnamo 2013. Wimbo huu ulipokelewa kwa kishindo kwa ajili ya mistari yake mizuri ya maudhui ya mapenzi na ulifanya vizuri sana katika redio mbali mbali za Tanzania.

Baada ya kuachia nyimbo kadhaa baadae aliungana na msani wa Nigeria Davido na kuachia ngoma ya “Number One” remix ambao ulikubaliwa na ulimwengu wote. Kisha alipata uteuzi wa Tuzo la BET wakati huo. Diamond ameendelea kushirikiana na wasanii zaidi ndani na njee ya Afrika kama vile Omarion, Rick Ross, Morgan Heritage, Tiwa Savage, Ne-yo, Koffi Olomide, Fally Ipupa na wengine wengi. Kwa sasa yeye ndio mkurugenzi mkuu wa WCB na anasimamiwa na Babu Tale, Sallam Sk na Said Mkubwa Fella katika Tasnia ya Muziki Tanzania.

Alianzisha lini studio za Wasafi Music na vituo vya habari na sanaa?

Diamond Platnumz ndiye mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa lebo kubwa Afrika mashariki Wasafi Classic Baby (WCB). Lebo hiyo ilikuwepo kwa muda mrefu kama studio ya mziki lakini ikageuzwa kuwa lebo mwaka mwa 2015 baada ya Diamond kuwasajili; Harmonize, Rayvanny, Mbosso, Rich Mavoko, Queen Darleen na Lava lava.

Baada ya kuzindua lebo, WCB ilianzisha timu ya kufanya upigaji picha na kureodi mziki lililoitwa Zoom Extra linalosimamiwa na mwelekezaji Kenny. Baadaye, alijitosa katika tasnia ya habari akianzisha Wasafi media ambayo sasa inajivunia kuwa na Wasafi Radio na Wasafi TV ambazo ni baadhi ya vituo vikubwa vya habari nchini Tanzania kwa sasa.

Diamond ana albamu ngapi?  

  • Lala Salama 2012
  • A Boy from Tandale 2018

Nyimbo Bora zaidi za Diamond Platnumz

  • Haunisumbui
  • I Miss You
  • Waah
  • The One
  • Yope Remix
  • Baba Lao
  • Inama
  • Sikomi
  • Jeje
  • Kanyaga
  • Iyena

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond, Mbosso Waachia Video ya Ngoma Yao 'Baikoko'

Diamond ana Tuzo ngapi?

Diamond ameteuliwa kwa Tuzo 28 za Muziki wa Hip-hop hadi sasa na ameshinda 22 kati ya hizo. Tuzo za Muziki za Tanzania

  • Tuzo 4 za Muziki wa Channel O
  • Tuzo ya Chaguo la Watu.
  • 2015 - Tuzo ya Muziki ya MTV Africa
  • Tuzo 2 za Muziki za MTV Ulaya
  • 2016 – Tuzo 3 za WatsUp TV Africa Music Video Awards
  • Tuzo 5 za AFRIMMA

Diamond ana Thamani ya kiasi gani?

Yeye ndiye mmiliki wa WCB Wasafi Records, Wasafi TV na redio. Ni mmoja wa wasanii tajiri Afrika Mashariki. Mnamo 2013, alikuwa msanii anayeuza zaidi kwa sauti na kampuni za simu kupitia Tanzania. Anakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 7.

Diamond Yuko kwenye mahusiano yeyote?

Diamond Platnumz kwa sasa hana uhusiano wowote wa kimapenzi, ila ana watoto sita kwa jumla na wanne ndio wanaojulikana. Awali, Diamond alikua na mahusiano na mwanabiashara kutoka Uganda Bi. Zari Hassan ambaye walifanikwa watoto wawili;Nillan na Tiffa. Kisha akapata mtoto kwa jina Dylan na Hamissa Mobetto. Baadaye akaingia kwenye uhusiano na dada kutoka Kenya Bi. Tanasha Donna amabye pamoja walipata mototo mmoja Naseeb Junior.

 

Leave your comment