Maua Sama Agadhabishwa na Zogo Kati ya Harmonize na Rayvanny

[Picha: Ghafla]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kwa siku kadhaa sasa zogo kati ya wasanii wa Bongo Harmonize na Rayvanny limeendelea kuvuja kufuatia kisa cha uhusiano wa Harmonize, Kajala mwanawe Paula na Rayvanny.

Katika sakata ambayo sasa Harmonize anatishia kuwashtaki watu kadhaa kwa kashfa ya kumchafulia jina, wasanii wengine bongo wamekerwa na matukio haya.

Soma Pia: Tembo Vs Chui: Harmonize, Rayvanny Waachia Nyimbo Mpya ‘Vibaya’ na ‘Nyamaza’

Maua Sama ameonyesha kugadhabishwa na kelele hizi akisema kuwa badala kuipa kelele hizo kipaumbele anasihi vyombo vya habari kucheza mziki.

Kwake, ubunifu na uwekezaji wa wasanii inapotea na kuwa migogoro kama hiyo ya hao wawili.

Kupitia mtandao wa Twitter Mau Sama alionyesha kukerwa na kutaja nyimbo zinafaa kuwa kwenye trends badala ya mgogoro huo.

“Marioo – For You Professor Jay- Utanambia nini Rosa Ree - Satan Billnass - Tatizo Mbosso - Baikoko Frida - Madam President I think they deserve more airtime than what’s trending currently. A  lot of creativity and investment inapotea/haikuzi sanaa ya Tanzania! Please give it a rest” aliandika Maua Sama.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Kali Kutoka Konde Music Worldwide Mwaka 2021

Katika kumuunga mkono Mimi Mars, Lulu Diva, Rosa Ree walipigia upatu mawazo ya Maua Sama.

Vile Vile, msanii mkongwe wa kike Ray C pia ameongezea sauti yake katika sakati hii ikiwasahi Harmonize na Rayvanny kutoaibishana mitandaoni.

Kwake Ray C anasema wasanii hao wanajulikana zaidi ya barani Afrika na aibu hizi zinashusha hadhi ya mziki wa Tanzania iwapo bado wanajaribu kushindana kimataifa katika sanaa.

 “Tunawakubali kinyama!! sema mnatuletea Pwagu na Pwaguzi Taarabu......Na nyie ni watoto wa kiume afu mko juu vibayavibaya....Sasa!!!.Wakati mnapoteza muda kushushana na kuabishana wenzenu wanabebana mpaka kwenye magrammy!!!Ukumbi mshaachiwa sasa msituzingue na nyie....” aliandika Ray C.

Leave your comment